Saturday, November 28, 2020

DULLAH MBABE: MCHINA ALIKAA, ITAKUA CHEKA!

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

TANZANIA imejaaliwa kuwa na mabondia wengi wa ngumi za kulipwa wanaochipukia na wa zamani, wakiwamo wale wanaotoka katika ukoo wa mzee Matumla, yaani Rashid, Mbwana, Hassan na wadogo zao.

Ndani ya miaka 10 kama si 20, kumeibuka mabondia wengi wenye uwezo wa hali ya juu, akiwamo Francis Cheka anayetakwa kuchangia kwa kiasi fulani kumaliza utawala wa familia ya mzee Matumla katika mchezo huo.

Mbali ya Cheka, kumeibuka mabondia wengine chipukizi ambao wamekuwa wakiwakilisha vema Tanzania kwenye mapambano mbalimbali na kuliletea sifa taifa letu.

Kati ya mabondia hao walioibuka huwezi kuliacha jina la Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ aliyeibuka kwenye kipindi hiki cha miaka ya karibuni na kujizolea umaarufu mkubwa.

Dulla aliyeanza ngumi mwaka 2013 na kuweka rekodi ya kushika nafasi ya 110 katika viwango vya dunia uzito wa ‘cruiser weight’, kati ya mabondia 1202, anashika nafasi ya 13 kwa ubora wa viwango vya Tanzania kulingana na viwango vya tovuti ya BoxRec.

Katika umri wake wa miaka 23, ameshacheza mapambano 18 ya ndani na nje ya nchi. Ameshinda 14 kati ya hayo 13 ya ‘knockout’, amepoteza manne kwa ‘knockout’ akiwa hajatoka sare hata mchezo mmoja.

Dullah kwa sasa anafuata nyayo za Francis Cheka japo kwa siku za karibuni ameamua kukaa pembeni, wengi wakiamini utawala wake umemalizika.

BINGWA limemtafuta Dullah Mbabe ili kuzungumzia masuala mbalimbali likiwamo lile pambano alilowaomba mapromota wamwandalie dhidi ya mpinzani wake Francis Cheka.

Pambano lake na Cheka

Siku chache baada ya bondia Francis Cheka kusema yupo tayari kupambana na Dullah Mbabe popote pale hata nyumbani kwake, bondia huyo ameibuka na kusema bado pambano hilo halijapata promota.

Awali promota Kaike Siraju alikuwa tayari kuandaa pambano ila anataka kulipeleka Morogoro jambo ambalo nimelipinga vikali.

“Kwa miezi hii miwili ya karibuni sina pambano lolote lile na leo toka asubuhi nipo kwenye kikao na baadhi ya mapromota, hilo la Cheka lilikuwapo ila kwa sasa limekosa mtu wa kuliandaa,” alisema.

Alisema kuwa pambano lake la mwisho amemchapa Mchina, Chengbo Zheng kwenye raundi ya kwanza tu na kushinda kwa KO pale kwenye Ukumbi wa Diamond Jublee.

Alipoulizwa zaidi kuhusu mpinzani wake, Cheka ambaye amejitapa kuwa tayari kwa lolote, Dullah Mbabe aligoma kuzungumzia na kuamua kukata simu huku alipotumiwa SMS hakuijibu mpaka tunakwenda mtamboni.

Amewahi kumtwanga Maugo

Dullah Mbabe kwenye rekodi zake anajivunia kumtwanga bondia mkongwe, Mada Maugo, kwa TKO raundi ya tatu katika pambano la ubingwa wa Afrika (light heavy weight) kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

 

Kitendo cha kumpa kichapo Maugo ni wazi kiliweza kumtangaza huku wengine wasiamini kile kilichotokea kwenye pambano hilo lililovuta hisia za watu wengi.

Umahiri alioonyesha kwenye pambano hilo uliweza kumfungulia njia mpya ambapo alipata mapambano mengine ya kimataifa kama lile la Mchina liliofanyika Oktoba mwaka huu.

Amewahi kupambana pambano la dunia 

Dullah Mbabe amewahi kupambana na Mjerumani Toni Kraft kwenye pambano la kuwania Ubingwa wa Dunia (WBC) ambapo Mtanzania huyo alipoteza.

Pambano hilo la raundi kumi lililofanyika kwenye Ukumbi wa Ballhaus Forum, Munich, Ujerumani, Mbabe alionekana kumdhibiti vilivyo mzungu huyo lakini matokeo ya jumla yalimpa ushindi Mjerumani huyo.

Usichokijua

Mada Maugo aliwahi kutangaza kumvunja taya Dullah Mbabe kwenye pambano lao na kumtaka kutafuta fedha za matibabu mapema, lakini matokeo yake alipigwa kwa TKO raundi ya tatu tu.

 

Rekodi

 Jina: Abdahallah Pazi

Mapambano:   19

Shinda:       14(K0 13)

Poteza:         4(KO)

Kuzaliwa: Mei 13 Mei 1993

Uzito: Kg 68, Creiser Weight

Urefu: 5’10/sm 178

Nchi: Tanzania

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -