Wednesday, January 20, 2021

DUNIA YA MKE WANGU

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Ilipoishia

WAKATI huo ilikuwa ni saa 6:00 usiku, Kai alivaa koti lake la jinsi. Alibeba vitu vyake vya kusafiria, pamoja na ile dawa ya kujikinga na virusi vya Ebola, aliyokuwa ameigundua siku mbili zilizopita akiwa Uingeraeza. Upesi alitoka nje. Aliwasha gari na kuondoka nyumbani. Hata mlinzi wake alishangazwa na kuondoka kwa bosi wake pale nyumbani. Maana hata alipomuaga Kai hakuitikia.

SASA ENDELEA

Aliendesha gari kwa kasi kuelekea uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere.  Hakujali kama atakosa usafiri wa ndege kwa wakati huo, ndege inayokwenda Addis Ababa Ethiopia. Alichojali yeye ni kuhakikisha anamuona mke wake tu.

Baada ya dakika 15, alifika uwanja wa ndege upesi alielekea mapokezi.

“Kuna ndege inayokwenda Ethiopia usiku huu?” aliuliza Kai akiwa anahema.

“Samahani kaka kwa muda huu hakuna ndege inayokwenda Ethiopia ni hadi pale saa moja asubuhi,” alijibu mhudumu.

“Mungu wangu!” aliongea Kai na kuondoka pale mapokezi.

Alirudi kwenye gari lake na kutulia. Kama mtu aliyezidi kuchanganyikiwa, alikuna kichwa chake muda wote, kama vile kilikuwa na chawa. Alilia mara kwa mara kama mtoto mdogo. Moyo wake uliwaka moto. Alitamani aote mbawa ili apae hadi pale alipo mkewe.

Alikesha pale pale hadi asubuhi. Saa 12:20 alikwenda kukataa tiketi ya kuelekea Addis Ababa Ethiopia. Saa 1:00 ndege ya Ethiopia airways iliondoka uwanja wa mwalimu Nyerere na kuanza kuitafuta ardhi ya Ethiopia.

Kai akiwa ndani ya ndege aliendelea kulia akimlilia Julia. Bado hakuamini mara moja kama kweli mkewe alikuwa na maambukizi ya virusi vya Ebola. Alihisi labda ule utani wa mkewe umerudi. Alihitaji kujiridhisha kuona kwa macho yake juu ya kile alichokuwa amekisema mkewe kilichopelekea yeye kupoteza  fahamu ghafla.

Aliujiliza, itakuwaje kama kweli mke wake atakuwa na maambukizi ya Ebola. Hakupata jibu la haraka, kwa  sababu, alijua mtu yoyote anaepatwa na ugonjwa huo, lazima apoteza maisha. Kwa kuwa hadi kufikia muda huo, dawa ya kutibu ugonjwa huo ilikuwa bado haijaptikana.

Yeye alikuwa amefanikiwa kugundua kinga ya ugonjwa huo, lakini dawa ya kuua virusi vya Ebola ndani ya mwili wa binadamu alikuwa bado hajafanikiwa kuigundua. Na hata hivyo, kinga hiyo aliyokuwa ameingundua kutokana na ndoto aliyokuwa ameiota, alikuwa bado hajaithibitisha vya kutosha kama kweli ilikuwa inamkinga mtu ipasavyo dhidi ya virusi vya Ebola.

Hakuwa tayari kumpoteza mke wake aliyefunga naye ndoa miezi mitano iliyopita. Mwanamke aliyekuwa akimpenda kuliko kila kitu alichokuwa nacho katika ulimwengu huu, kuliko hata kipaji chake cha sayansi, kipaji kilichobeba umaarufu na furaha yake ya maisha kabla hata hajakutana na Julia.

Alizidi kumuomba Mungu atende muujiza mwingine wa kumuokoa mke wake kule aliko. Alijisemea kuwa hata kama mke wake atakuwa na maambukizi hayo, lazima atarudi naye nyumbani.

Hakuwa tayari kuona anamuacha mke wake katika nchi hiyo, nchi iliyokuwa na maambukizi ya kutisha ya ugonjwa huo.

Saa nane mchana, ndege ya Ethiopia Airways ilitua uwanja wa kimataifa wa Addis Ababa. Kai alikuwa wa kwanza kushuka kwenye ndege hiyo. Alitembea haraka kuelekea sehemu ya ukaguzi. Baada ya muda, alitoka nje ya uwanja huo ambapo alielekea moja kwa moja hadi sehemu ya maegesho ya tax.

“Upesi nipeleke hoteli yoyote nzuri,” aliongea Kai, mara baada ya kuingia kwenye gari.

Dereva aliwasha gari na kumpeleka kusini mwa jiji hilo kwenye hoteli moja iliyoitwa  Kavenda Nuki iliyokuwa karibu na ubalozi wa Uingereza.

Mara baada ya kuingia katika chumba cha hoteli, Kai aliwasha runinga, huku akiendelea kupanga vitu vyake kwa ajili ya safari ya kuelekea katika mji wa Amhara. Hakujali kama atapata maambukizi au hata pata. Yeye alichojali ni mke wake maana ndiye aliyekuwa akimpa furaha ya kuishi katika dunia hii.

Wakati huo televisheni ya taifa ya Ethiopia ilikuwa ikiendelea kutangaza hali ya hatari katika nchi hiyo. Taarifa ya kituo hicho ilisema kuwa, ugonjwa wa Ebola umekwisha kuua zaidi ya watu 2,00000 katika taifa hilo. Mji pekee uliokuwa umebaki salama ni mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa, hata hivyo nao ulikuwa kwenye tishio kubwa la kuvamiwa na ugonjwa huo.

Taarifa hiyo pia ilileta habari ya dunia iliyozidi kutangaza hali ya hatari katika pande zote za dunia. Tayari ugonjwa wa Ebola ulikuwa umeiingia katika mabara yote saba. Katika Bara la Asia tayari watu 100 walishakuwa wamepoteza maisha, huku zaidi ya 800 wakiwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo. Barani Ulaya watu 20 walishakuwa wamepoteza maisha na wengine 90 wakigundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

Nini kitaendelea? Usikose Alhamisi

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -