Saturday, January 16, 2021

DUNIA YA MKE WANGU

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Ilipoishia

ALIJUA pia huenda mkewe asife kwa Ebola tu bali hata kwa njaa. Aliongeza mwendo akizidi kulikaribia eneo lililoitwa Labula. Labula lilikuwa ni eneo la  watu wabaya wa kijiji hicho waliokuwa wakifanya kazi ya kuwateka watu na kuwafanyia vitendo viovu.

SASA ENDELEA

Alianza kuhisi harufu kali ya maiti kabla hata hajarikaribia eneo la Labula. Hakika hali ya kuogopesha ilimtawala kuanzia kichwani hadi miguuni. Hakuogopa kuambukizwa virusi wala kufa kwa njia yoyote ile. Hofu yake ilikuwa ni juu ya mkewe. Hali halisi aliyokuwa akizidi kuiona katika kijiji hicho, ilianza kumuaminisha kuwa Julia hakuwa mzima.

Hofu ilikuwa kubwa kwa sababu, hakujua mke wake alikuwa katika hatua gani kati ya zile tatu za kuugua. Ugonjwa wa Ebola ulikuwa na hatua tatu pindi unapokuwa umemuingia binadamu. Hatua ya kwanza mtu alikuwa anaweza kufanya kazi zake vizuri. Kwa sababu virusi vinakuwa bado havijaanza kuzaliana vya kutosha, lakini hutokwa na matone ya damu puani na baadae masikioni. Hatua ya pili mtu huanza kuishiwa nguvu na kupatwa na homa kali huku damu zikimvuja sehemu zote zenye matundu. Na hatua ya tatu baadhi ya viungo vya mwili wake huanza kuoza maana chembe hai za damu hushindwa kupigana na virusi zaidi elfu hamsini.

Mazingira ya kijiji cha Keneza yalishindana na moyo wa Kai, moyo uliokataa kuamini kuwa mke wake alikuwa amekwisha kufa. Machozi hayakukauka muda wote, licha ya kujikaza kiume. Alilia sana kwa kuwa, tabasamu la Julia lilikuwa limeiteka akili yake.

Alifika eneo la Labula na kukutana na maiti nyingi. Baadhi ya maiti zilikuwa zimetundikwa kwenye miti. Hakujua ni kwanini ilikuwa vile. Hakutambua kuwa, baadhi ya kikundi kibaya kilichokuwa kimekitawala kijiji hicho, ndicho kilichokuwa kimetekeleza mauji hayo. Hata hivyo watu wa kikundi hicho nao walishakufa muda mrefu kutokana na Ebola kuwashambulia wote kila kona.

Kai alifunga breki za gari na kushuka. Alipita kwenye maiti akaelekea ndani ya nyumba moja iliyokuwa na baadhi ya vitu. Alishtuka baada ya kuyaona mavazi ya Letc, mavazi yaliokuwa maalumu kwa madaktari wanaotoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola. Alianza kuchanganyikiwa zaidi akijua kuwa mke wake naye alikuwa ni miongoni mwa watu waliokufa katika eneo hilo.

Kama kichaa alianza kugeuza geuza maiti. Akizikagua moja baada ya nyingine ili kuona kama atamkuta kipenzi mke wake. Hakufanikiwa kumuona. Julia hakuwa miongoni mwa zile maiti.

Akiwa nje ya ile nyumba, alishangaa kuona alama za magurudumu ya gari, zikiwa zimeelekea upande wa kulia. Upesi aliingia kwenye gari, akaliwasha na kuifuata ile njia ambayo hakujua inaelekea sehemu gani ya kijiji hicho.

Kai hakujua kama lori alilokuwa ameliona kule Amhara, ndio mahali alipokuwa mkewe. Hakulifikiria kabisa hata kuwa na hisia nalo. Aliamua kuifuata ile njia ya vumbi akiendesha gari kwa kasi.

Baada ya nusu saa, alifika eneo lililoitwa Keneza Mweka. Eneo hilo lilikuwa ni eneo  maalumu kwa ajili ya ibada za mizimu. Wanakijiji wa Keneza walikuwa wakiamini shida zao hutatuliwa hapo. Hata watu wa vijiji vinavyokaribiana na mpaka wa Etthiopia na Somalia walikuwa wakija kufanya ibada mahali hapo. Eneo hilo lilikuwa na zaidi ya kilomita 130 likienda kukaribiana na mpaka wa Amhara na Ethiopia.

Kai aliposogea mbele alichanganyikiwa zaidi baada ya kuona maiti zisizohesabika zaidi ya watu 80000 walikuwa wamepoteza maisha. Watu hao walifia eneo hilo kwa sababu, walikuwa wakiamini mizimu itawalinda dhidi ya Ebola waliamua kujenga makazi wakiomba mizimu usiku na mchana. Lakini hata hivyo, Ebola iliwatafuna vibaya, kuanzia nchi nyingine ya Somalia, hadi pale alipo. Maana ugonjwa huo ulishakuwa umeua wengi kuanzia Mogadishu Somalia hadi Ethiopia.

Kai alishtuka baada ya kuona baadhi ya watu wakiwa wamekufa huku wakiwa wamevaa mavazi ya kiuuguzi na kidaktari. Akili na nafsi yake vilianza kuteswa na taa nyekundu.

Kuanzia mwanzo wa mipaka ya Ethiopia, hadi nchi za jirani, maiti zilikuwa zimetapakaa juu ya ardhi. Huku harufu mbaya ikiendelea kuharibu hali ya hewa ya maeneo hayo, kwa sababu mwili wa binadamu ukishaoza ni chukizo kubwa kwa pua inayopenda kuhisi halafu nzuri.

Hali hiyo ilizidi kumuogopesha Kai na kumfanya ajione kama yuko kuzimu. Alipiga hatua za haraka, na kuanza kuutafuta mwili wa Julia mke wake kipenzi, sasa akiamini mke wake alikuwa amekwisha kufa. Japo alikuwa akihitaji utulivu mkubwa katika kufanya hivyo. Hurufu kali iliyosambaa kutokea katikati ya nchi nyingine hadi ile aliyopo, ilimfanya kuzikagua maiti kwa tabu na kwa haraka sana.

Hakika ugonjwa wa Ebola ulikuwa unakwenda kummaliza kabisa binadamu anayeishi Afrika na yule anayeishi pembeni ya bara hilo. Hakuna binadamu aliyekuwa hai eneo hilo.

Kai alikuwa akilia muda wote, ingawa alikuwa amejichoma sindano ya kujikinga na ugonjwa huo, alimjali zaidi mke wake.  Alilia kwa sababu, juhudi ya kumtafuta mke wake aliyokuwa ameifanya kwa kila hali, ilishindwa kumuaminisha kuwa Julia alikuwa mzima. Shauku yake ilikuwa ni kutaka kumuona mke wake akiwa hai au akiwa amekufa. Kitu kilichokuwa kikimuuma zaidi ni juu ya ujauzito aliokuwa nao Julia. Alichanganyikiwa na kuumia zaidi akijua kuwa mke wake alikuwa amekufa akiwa na mapacha wake tumboni.

Hakujali kama kinga aliyokuwa ameigundua siku nne zilizopita London Uingereza ilikuwa imefanikiwa kumkinga au haikufanikiwa. Hakuona umhimu wa kuishi bila kuwa na mke wake. Aliona ni sawa hata akipatwa na virusi.

Baada ya kumtafuta Julia kwa muda mrefu kwenye maiti zenye mavazi ya kidaktari na kushindwa kumpata, alirudi kwenye gari na kukaa. Alilia akimuomba Mungu msamaha kwa kushindwa kumlinda Julia kama alivyokuwa amemuahidi.

Akiwa amechoka kulia, huku akilitazama eneo lote lilofunikwa na maiti, alimkubuka padre wa kanisa aliyekuwa amemuacha kule kanisani Mulungo Keneza. Alikumbuka kuwa padre huyo alimwambia kuwa, kama Julia hakukwama eneo la Labula basi alikwama mpakani.

Kai alishtuka, upesi aliwasha gari na kugeuza kurudi alikotoka. Aliendesha gari kurudi katikati ya kijiji cha Keneza. Alitembea kwa mwendo wa kilomita 10 hadi alipolirudia eneo la Labula.

Alikata kulia na kunyosha barabara inayolekea mjijni Amhara. Baada ya dakika 15, alikuwa anaingia kwenye barabara ya lami. Aliendesha gari kama kichaa hakujua kama kuna kupata ajali. Moyoni alijisemea kuwa kama anakosea kumpenda Julia kiasi kile Mungu amsamehe.

Akiwa anaendelea kukanyaga mafuta, alijiuliza kuwa eneo la mpaka analolirudia kwa mara ya pili, mke wake alikuwa sehemu gani pale maana eneo lote nalo lilikuwa na maiti, maiti za watu waliouawa na jeshi la Ethiopia. Alijipa imani kuwa eneo lile anaweza kuona mwili wa mkewe japo hakuwa amethibitisha kuwa Julia alikuwa amepoteza maisha.

Baada ya masaa sita, akiwa ameupita mji wa Amhara, alikuwa akiukaribia mpaka wa Amhara na Addis Ababa. Akiwa anazidi kusogea, mbele yake aliliona lile  lori alilokuwa ameliona mwanzo pindi alipokuwa akipita kuelekea kijiji cha Keneza kilichopo Amhara.

Nafsi yake ilishtuka, mapigo ya moyo wake yalimdunda, alianza kuhisi kitu cha tofauti. Wakati huo huo akijilaumu kimoyo moyo kuwa kwanini alilipuuza lile lori  pindi alipokuwa akipita.

Aliendesha gari kwa kasi, akalitoa barabarani na kulipeleka kule lori lilipokuwa. Alipofika kwenye lori alifunga breki. Upesi alishuka na kulitazama lori pande zote. Pembeni ya lori hilo aliziona nembo za umoja wa mataifa pamoja na ile ya Shirika la Afya Duniani (WHO) akili yake ilianza kufikiria kuwa mke wake alikuwa mahali pale.

Alielekea upande wa dereva ambapo hakumuona mtu yoyote zaidi ya damu zilizokuwa kwenye kiti zikionyesha kuwa zilimwagika wiki mbili zilizopita.

Aligeuza na kupiga hatua kuelekea nyuma ya lori. Wakati huo moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali kupita siku zote. Alihisi yuko kwenye mateso makubwa yasiyokuwa na mfano. Alianza kumuomba Mungu pindi alipokuwa akipiga hatua za uoga kuelekea nyuma ya lori. Moyo wake ulisema kuwa unaomba umuone Julia ndani ya gari hilo hata akiwa maiti.

Nini kitafuatia usikose kesho   

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -