Sunday, November 29, 2020

EL CLASICO: MADRID WANATAKA KUWAZIDI POINTI TISA, BARCELONA WAPANIA KUPUNGUZA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

BARCELONA, Hispania

KLABU ya Barcelona watakuwa na mtanange wa El Classico dhidi ya mahasimu wao, Real Madrid, kesho kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Vita hiyo inatarajiwa kuwa kubwa kutokana na kila klabu kupania kuongeza ama kupunguza pengo la pointi wanazopishana kwa sasa.

Real Madrid wanaweza kuongeza pengo lao la pointi na kuwa tisa na kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa La Liga kama wakifanikiwa kuwafunga Barcelona watakaokuwa wakipambana kupunguza pengo hilo na kuwa pointi tatu  na kuharibu rekodi ya Madrid ya kutokufungwa msimu huu.

Ushindi kwa upande wa Madrid utaendelea kuwapa nafasi nzuri ya kunyakua taji hilo la La Liga msimu huu.

Miamba hiyo ya mjini Madrid itaingia kwenye mchezo huo wa El Classico ikiwa timu tishio kwa sasa Ulaya, baada ya kucheza mechi 31 kwenye ligi bila ya kufungwa.

Tangu timu hiyo ianze kunolewa na kocha Zinedine Zidane msimu uliopita, wamepoteza mechi moja pekee katika mechi 33, wakishinda mechi 27 na kutoka sare tano.

Kwa upande wa mahasimu wao Barcelona, msimu huu wamekuwa na kiwango kibovu ambapo mwishoni mwa wiki, walibanwa na Real Sociedad na walikuwa na bahati kupata pointi kwenye mechi hiyo.

Mbaya zaidi ni matokeo ya mechi yao ya mwisho, ambapo Madrid waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye uwanja huo wa Camp Nou.

Neymar na Luis Suarez wamekuwa kwenye kiwango kibovu, lakini kurejea kwa Iniesta kunaweza kuongeza nguvu Barcelona inayoonekana kuwa timu ya kawaida bila ya nyota huyo.

Lakini pamoja na ujio wa Iniesta, kiwango cha Neymar, Suarez na Messi na jinsi ukuta wa Real Madrid ulivyojengeka, ni wazi kwamba bado Barcelona watakuwa na wakati mgumu na kuna uwezekano mkubwa wa Real Madrid kuibuka na ushindi japo mdogo kwenye mchezo huo wa kesho na kuwapa nafasi nzuri ya kunyakua taji lao la kwanza la La Liga baada ya miaka mitano kupita.

Moja ya jambo ambalo wengi wanalitarajia katika mechi za miamba hiyo miwili ni mabao, Novemba mwaka 2002 ilikuwa ni mara ya mwisho kwa miamba hiyo kukutana na kutoka sare ya 0-0, hivyo katika mechi 26 zilizopita nyavu zimeweza kutingishika.

Pamoja na mabao lakini tutarajie fujo katika mechi hiyo ya El Clasico ambapo hilo limekuwa jambo la kawaida kila wanapokutana.

Katika mechi nne za mwisho za La Liga, kulikuwa na kadi za njano 29 na nyekundu mbili ambazo zimeonyeshwa katika mechi mbili za mwisho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -