Wednesday, October 28, 2020

EL CLASICO NI VITA YA WAFALME WA BALLON D’OR

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MADRID, Hispania

UNAWEZA kusema kama ni vita ya tuzo ya mchezaji bora wa dunia wakati utakapokuwa ukiizungumzia mechi itakayoikutanisha miamba miwili ya soka nchini Hispania, Real Madrid na Barcelona, katika michuano ya Ligi Kuu nchini humo, La Liga.

Msemo huo unatokana na kwamba vinara hao,  Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, wanashuka uwanjani huku wakiwa kwenye orodha ya nyota wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d’Or.

*HABARI ZA KILA TIMU

Barcelona

Baada ya kuwapumzisha nyota wake kadhaa wakati wa mechi ya Kombe la Mfalme, Copa Del Rey dhidi ya Hercules, mechi hii ya leo, Luis Enrique atapanga kikosi imara dhidi ya Los Blancos.

Mbali na kupanga kikosi imara, pia habari nyingine nzuri kwa mashabiki wa timu hiyo hakuna majeruhi mpya katika mtanange huo muhimu.

Kurejea kwa nyota wao, Lionel Messi, Luis Suarez  na  Neymar Jr kunaweza kuleta madhara makubwa katika safu ya ulinzi ya Real Madrid na hivyo kumfanya  Kocha  Zinedine Zidane  kuwazuia wakali hao ambao wanasemekana kuwa ndio safu bora ya ushambuliaji  katika  ulimwengu wa sasa wa soka.

Kwa upande mwingine, katika safu ya beki wa kati kwa sasa Barcelona nako inaonekana kuwa itakuwa imeimarika kutokana na nyota wao, Gerard Pique na  Javier Mascherano watakuwa katika ubora wao kwa ajili ya kuzima mashambulizi ya  Real Madrid.

Pia kurejea kwa nahodha wao, Andres Iniesta, ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili inaweza kuwa msaada mkubwa kwa vinara hao wa  Catalans.

Msimu huu Barcelona ilikuwa inakabiliwa na tatizo la nyota wao, Sergio Busquets, kucheza kwa kiwango cha chini, lakini ujio wa Iniesta mambo yanaweza yakawa mazuri zaidi kwao.

*Mfumo; leo Barcelona inaweza kutumia mfumo wa  4-3-3, ikiwachezesha  Marc-André,  Roberto, Pique, Mascherano, Alba – Rakitic, Busquets, Iniesta – Messi, Suarez, Neymar.

 *Real Madrid

Msimu huu Real Madrid imekuwa na mkosi wa kukosa nyota wao muhimu kutokana na kuwa majeruhi.

Katika mchezo huu wa leo, vinara hao watamkosa staa wao, Gareth Bale, ambaye anakabiliwa na matatizo ya enka na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili na huku ikiwa tayari kiungo wao, Toni Kroos, naye akiwa nje.

Mbali na mastaa hao, pia nyota mpya ambaye kwa sasa amekuwa akicheza kwa kiwango kizuri akiwa na kikosi hicho cha Los Blancos, Alvaro Morata, hatakuwamo kwenye mtanange huo baada ya kuumia akiwa na timu ya taifa.

Hata hivyo, habari njema kwa Zinedine Zidane ni kwamba kiungo wao, Casemiro, amesharejea kikosini baada ya kuwa nje kwa muda wa wiki kadhaa.

Wiki za hivi karibuni mashabiki wa  Real Madrid wamekuwa wakimwaga tabasamu kutokana na nyota wao, Ronaldo, kurejea kwenye ubora wake ambapo Mreno huyo amekuwa akicheka na nyavu katika michezo muhimu na leo ndiye atakuwa tegemeo lao.

*Mfumo; Real Madrid inaweza kutumia mfumo wa 4-3-3, ikiwatumia nyota wake, Navas, Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric, Kovacic, Casemiro, Isco, Ronaldo, Benzema.

Dondoo za mechi zilizopita

Messi vs. Real Madrid

 • Messi ndiye mfungaji bora katika historia ya mechi za El Clasico, akiwa na mabao 21.
 • Messi ametoa pasi zilizozaa mabao 13 kati ya 32 dhidi ya Real Madrid.
 • Ameshinda 15 za El Clasico, sawa na asilimia 47
 • Messi amefunga asilimia ya mabao 57 akiwa
 • Messi hajawahi kufunga bao katika mechi tano za El Clasico zilizopita.

Ronaldo vs. Barcelona

 • Kama ilivyo kwa Messi, Ronaldo amefunga mabao mengi akiwa ugenini kuliko akiwa nyumbani, hadi sasa amefunga 10 kati ya 16 ya El Clasico aliyofunga akiwa Camp Nou.
 • Ni mchezaji Alfredo Di Stefano ambaye amewahi kufunga mabao 18 dhidi ya Barcelona, akiwa na Real Madrid anayemzidi Cristiano.
 • Ronaldo ana rekodi ndogo ya kuondoka na ushindi dhidi ya Barca, ambapo ameshinda saba kati ya 25 alizocheza, sawa na asilimia 28.
 • Mreno huyo amewahi kutoa pasi moja iliyozaa bao katika mechi 25 za El Clasico, idadi ambayo ni chini kwa mechi 12 dhidi ya Messi.

*Takwimu muhimu

 • Real Madrid hawajafungwa katika mechi 31 za mashindano.
 • Real Madrid wameshinda mechi ya hivi karibuni ya El Clasico walipoifunga  Barca 2-1.
 • Barcelona haijawahi kufungwa katika mechi 29 kati ya 32  za La Liga ilizocheza ikiwa nyumbani.
 • Straika wa Barca, Messi, hajawahi kufunga bao katika mechi za  El Clasico tangu mwaka

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -