Monday, January 18, 2021

ELIMU NA UKWELI KUHUSU MAPENZI HALISI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

DUNIANI kuna mambo mengi sana ya kuyaamini. Halikadhalika kuna mambo mengi yasiyofaa kuaminiwa. Ila kwa bahati mbaya wengi wanaamini tofauti na ukweli.

Wapo wanaoamini kuna mahali wanapendwa kumbe hapana, pia kuna wengine wana mashaka na mahali wanapopendwa kweli wakati walitakiwa kujiachia na kuona fahari kuwa na watu walio nao katika mahusianio yao.

Najua umeshawahi kusikia mengi juu ya mapenzi na suala la elimu. Najua hata wewe pia kuna kitu unaamini kuhusiana na suala hilo. Sitashangaa kama ukiamini kuwa elimu ni suala la muhimu sana kuangalia wakati wa kuoa au kuolewa.

Huenda ukawa unaamini kuwa kama una ‘Masters’ basi vyema ukampata wa elimu wa kiwango chako. Unajua kwanini sitashangaa?

Kwa sababu imekuwa kawaida vitu visivyo na ukweli kuaminiwa na kuenziwa. Ushawahi kujiuliza kuwa kwanini unaangalia elimu kama suala muhimu  kabla hujaingia katika  ndoa?

Bila shaka huenda ukawa unamini ukiwa na mtu wa kiwango kikubwa cha elimu basi kila kitu baina yenu kitakuwa safi. Ila kimsingi hapa itakuwa umeongea kuhusiana na uwezo wa kufikiri wa mtu ila utakuwa umeujumlisha katika suala la elimu. Hapa sidhani kama utakuwa sahihi.

Maana wengi mnapozungumzia elimu mnakusudia ‘form education’ na si maarifa ya kumpa mtu mwangaza wa kutafsiri mambo katika ukubwa na maana inayostahili. Kama ni suala la maarifa bila kujali elimu (vyeti) linaweza kuwa lipo kwa mtu yeyote mwenye kiu ya kujua mambo na mfuatiliaji wa kina.

Pia ikumbukwe katika suala la mapenzi na ujenzi wa familia ya amani na upendo inahitajji watu wawe na hisia za kweli kwa kila mmoja. Hata ikiwa mna elimu kubwa za kiwango kimoja ila upendo ukikosekana baina yenu, hakutakuwa na utulivu wala familia iliyo bora.

Kwa maneno mengine ni kwamba, ikiwa unahitaji familia bora na ya amani kikubwa kuliko vyote ni kuangalia mtu anayekupenda na kukujali kwa maana huyo ndiyo anayeweza kukusikiliza, kukushauri vizuri na  akakupa amani. Bila kujali elimu utaifa wala kabila analotoka. Ni wangapi walio na elimu kubwa zinazofanana na kila kitu baina yao hakiko sawa? Ni wengi!

Suala la elimu ni muhimu sana ila katika mapenzi muhimu zaidi ni hisia za upendo katika nafsi zenu. Kwa kupenda kuangalia mambo haya ya kujinasibisha katika jamii leo mahusiano mengi yamebaki jina na wahusuka hawana hisia na wenzao. Elimu itabaki kua elimu na hisia zitabaki kuwa hisia.

Leo unakuta katika jumba kubwa lenye kuvutia nje, ndani amani hakuna. Mzee anatoka na kidosho na mama anatoka na dereva wake. Wakati mwingine si vyema kuhukumu kuwa ni umalaya ila pia ni vyema zaidi kama tutaangalia sababu za haya kutokea.

Binaadamu huwa ana kawaida ya kutaka kupata sifa na fahari katika jambo fulani. Na kama ukiendekeza hali hii katika mapenzi ndipo hapo utaamua kumchukua Agness kwa sababu wote mlihitimu Mzumbe, ukiamini kuwa atakuja kuwa mwema katika maisha yako. Ni hapa ndipo panapozaliwa ndoa tata na za kila mmoja kujiona yuko juu.

Katika mapenzi ya kweli kuna heshima na kujaliana. Bila kuangalia viwango vya elimu ila kama kila mmoja ana hisia za kweli na mwenzake kila mmoja atajiona yuko chini ya mwenzake. Kwa kawaida na hali ilivyo ndani ya dunia ya kweli ya mapenzi huwa hakuna madaraja. Yaani japo wewe ni masikini na umeolewa na tajiri ila kwa kuwa anahisia za kweli na wewe basi atajivunia zaidi wewe kuliko utajiri wake. Na katika hali hii ndipo hata suala la elimu kwa wapendanao huwa si kitu sana. Maana wakiwa ndani huwa wanaongea lugha moja na yenye kufanana.

Ndoa ni taasisi inayohitaji uwekezaji wa hisia zako na si elimu, kama unaamini anakupenda kwa dhati, uangalie huo upendo wake na si elimu. Kwa maana usikivu na amani katika mahusiano huwa inajengwa na watu wenye kupendana. Hapo ndipo watu wanaweza kusikilizana na kuelezana, hapo ndipo kuna kufundishana na kuelewana.

Ila kama hana hisia na wewe hata kama ana elimu kama nani, bado hatakuelewa. Na kutokuelewa huko si kwa sababu ya kitu kingine. Ila kwa kuwa huna nafasi katika nafsi yake. Nafasi ndogo wapendwa.

ramadhanimasenga@yahoo.com 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -