Thursday, October 22, 2020

EMERY AMPA NENO LA FARAJA OZIL

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LONDON, England


KOCHA Unai Emery amempa neno la faraja staa wake, Mesut Ozil, akisema kuwa katika maisha ni lazima uandamwe na lawama kama zinazomkuta staa huyo, baada ya kutangaza kuitema timu ya taifa ya Ujerumani, lakini akamwambia kwamba mashabiki wote wa klabu hiyo wapo nyuma yake.

Ozil alitangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa mapema mwezi uliopita kwa kile kiungo huyo anachodai ni kubaguliwa na viongozi wa Shirikisho la Soka Ujerumani (DFB), mashabiki na hata wanasiasa, baada ya kukutana na Rais wa Uturuki,  Recep Tayyip Erdogan.

Mbali na hao, pia viongozi wa ngazi ya juu katika soka la Ujerumani wamekuwa wakiyaponda madai hayo ya Ozil, huku Rais wa Bayern Munich,  Uli Hoeness, akiwa miongoni mwa wanaomponda staa huyo.

Hata hivyo, kocha huyo wa Arsenal alisisitiza jana kuwa Ozil anaungwa mkono na mashabiki wote wa Gunners kabla ya mchezo wao wa leo wa Ligi Kuu England dhidi ya West Ham.

“Tupo mahali hapa kumsaidia,” Emery aliwaambia waandishi wa habari. “Tupo kama familia na klabu hii ndiyo nyumbani kwetu. Katika kazi zetu kama makocha na wachezaji ni lazima tuishi kwa kupokea lawama. Tunapofanya vizuri watatuzungumzia vizuri. Wakati tunapofanya vibaya lawama lazima ziwe juu yetu,” aliongeza kocha huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -