Friday, November 27, 2020

England 0-0 Slovenia Mambo haya ndiyo yaliyojiri

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

HATIMAYE timu ya Taifa ya England, Three Lions, ilishindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018.

Kabla ya mtanange huo England walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kuibuka kidedea, lakini matokeo ya kutofungana ndiyo yaliyoamua mchezo huo.

Hii ni mara ya kwanza kwa England kukosa ushindi katika michezo ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali hizo kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu.

Hata hivyo, katika mechi ya juzi ambayo England walikuwa ugenini, makala haya yanaangazia mambo yaliyojitokeza hasa kwa upande wa Three Lions ambao walikuwa wakibashiriwa kuibuka na ushindi.

Hart aling’ara

Kwa kiasi kikubwa Hart alikuwa siri ya mafanikio ya England kupata matokeo hayo.

Kocha wa muda wa England, Gareth Southgate, anatakiwa kumshukuru mlinda mlango huyo kwani aliokoa mabao mengi ya wazi.

Aliokoa hatari mbili ambazo zilisababishwa na pasi mbovu alizopewa na Eric Dier na Jordan Henderson.

Rooney hapaswi kulaumiwa

Katika siku za hivi karibuni, Wayne Rooney ameonekana kushuka kiwango.

Licha ya kuwa nahodha wa timu yake hiyo ya England, Wayne Rooney hakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kilichoivaa Slovenia.

Hata hivyo, kuwekwa benchi kwa Rooney katika mchezo huo hakukuwa na manufaa kwa England.

Ni wazi Rooney si tatizo pekee la England, kwani hata kutocheza kwake hakuoneshi kuwa kumepunguza ubovu wa England.

Katika eneo la kiungo, Dier hakuwa kwenye kiwango kizuri na huenda hilo limetokana na kitendo cha kuingia mara moja pekee kwenye kikosi cha kwanza kwa kipindi cha wiki sita zilizopita.

Kukosekana kwa Rooney hakukutibu tatizo la England, ambapo kama ilivyokuwa chini ya Roy Hodgson, washambuliaji wa pembeni walionekana kutokuwa na msaada.

Lakini pia, staa Dele Alli alishindwa kuelewana na Daniel Sturridge.

Stones ni ‘mfalme mpya’ England

Kwa ujumla England haikucheza vizuri. Wachezaji walionekana kuwa wazito kuhamisha mipira kutoka langoni mwao na kwenda kushambulia.

Lakini John Stones alikuwa wa kipekee katika kikosi cha Three Lions.

Katika pasi 78 alizopiga ni nne pekee ambazo hazikuwafikia walengwa.

Alionesha uwezo huo huku akiwa ni mchezaji pekee wa kikosi cha sasa cha England ambaye hakucheza Euro 2016.

Walcott bado hakijaeleweka

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, amekuwa kwenye ubora wa hali ya juu pale Arsenal.

Hata hivyo, juzi alikuwa miongoni mwa mizigo katika kikosi cha England.

Katika mchezo huo, Walcott alitoa pasi 17 pekee. Kwa kiwango hicho, staa huyo alikuwa ndiye mchezaji aliyepiga pasi chache kuliko wote.

Akishambulia kutoka pembeni, mkali huyo alishindwa kuhamishia uwezo anaouonesha akiwa na Gunners.

Baadaye aliitwa benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Andros Townsend, ambaye alionekana kuipa uhai England.

England wana safari ndefu

Baada ya England kutolewa kwa aibu na ‘vibonde’ Iceland kwenye michuano ya Euro 2016, kocha wa timu hiyo, Hodgson aliachia ngazi.

Miaka miwili iliyopita kikosi hicho cha Three Lions kilivurunda nchini Brazil katika fainali za Kombe la Dunia.

Mashabiki wa England wanataka kuiona timu yao ikifanya vizuri lakini Hodgson na Sam Allardyce waliwahi kukiri kuwa ‘kuna matarajio makubwa kuliko hali halisi’.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -