Saturday, October 31, 2020

ENRIQUE AMFAGILIA DE GEA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

 LONDON, England


 

KOCHA wa timu ya Taifa ya Hispania, Luis Enrique, amemfagilia mlinda mlango wake, David de Gea, akisema kwa sasa ndiye bora duniani baada ya nyota huyo wa  Manchester United kuonesha kiwango kizuri kilichowasaidia kuondoka na ushindi wa mabao  2-1 dhidi  ya  England, katika mchezo wao uliopigwa usiku wa kuamkia jana katika Uwanja wa  Wembley.

Katika mchezo huo, De Gea ndiye aliyemhakikishia ushindi wa kwanza Luis Enrique ulioipa  La Roja pointi zote tatu baada ya kuokoa  shuti ambalo lingemfanya Marcus Rashford asawazishe kipindi cha kwanza na kisha akaokoa bao la wazi dakika za mwisho za mtanange huo.

Katika dakika hizo, Danny Welbeck alishayafanya matokeo kuwa  2-2  alipokwamisha mpira kimiani, lakini bao hilo likakataliwa baada ya kumfanyia madhambi  De Gea  wakati aliporuka kunasa mpira.

Ikiwa ni baada  ya kulaumiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa Hispania waliofanya vibaya katika fainali za Kombe la Dunia na kutolewa hatua ya 16 bora, lakini kiwango alichokionesha De Gea dhidi ya  England ikashuhudiwa akimwagiwa sifa na kocha huyo, Luis Enrique.

“Nina furaha ya pekee kwa kiwango alichokionesha  David,” alisema kocha huyo katika mkutano  na waandishi wa habari mara baada ya mechi hiyo.

“Yeye ni kati ya walinda mlango bora duniani na amekuwa akilidhihirisha hilo wiki hadi wiki katika michuano ya Ligi Kuu England. Sijawahi kuwa na wasiwasi naye katika hilo na wakati mwingine makosa huwa yanakusaidia kuimarika zaidi,” aliongeza kocha huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -