Wednesday, January 20, 2021

ERASTO NYONI HATARI SANA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

AMA kweli Simba hawajakosea kumsajili beki kiraka, Erasto Nyoni kutoka Azam FC, kwani katika michezo miwili ya Ligi Kuu aliyocheza mpaka sasa, amefunga bao moja huku akitoa pasi nne za mabao.

Nyoni alifunga bao lake hilo kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 7-0, ukichezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Ndiye aliyefunga bao la saba katika dakika ya 85, huku akisaidia kufungwa kwa mabao mengine mawili katika dakika ya 42, akipiga krosi iliyomaliziwa kiulaini na Shiza Kichuya na baadaye akatoa pasi nyingine kwa Juma Luizio akafunga.

Katika mchezo wa juzi uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, ambapo Simba walilazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Mbao FC, Nyoni ndiye aliyesaidia mabao yote mawili ya wekundu hao wa Msimbazi.

Alipiga krosi nzuri katika dakika ya 16, ikatua kwenye kichwa cha Shiza Kichuya na mpira kujaa wavuni moja kwa moja na baadaye akapiga tena krosi iliyounganishwa na James Kotei na kujaa wavuni.

Takwimu hizo zinaonyeshwa wazi kwamba Nyoni ni moja ya mabeki wanaojua wajibu wao ndani ya uwanja, kwani mbali na kuhakikisha anawazuia washambuliaji wa timu pinzani, pia yupo makini kusaidia kupatikana kwa ushindi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -