MUNICH, Ujerumani
BEKI wa pembeni wa Bayern Munich, Philipp Lahm, haamini kuwa wamefikia ubora wanaoutaka wakiwa chini ya kocha Carlo Ancelotti.
Kauli ya nyota huyo imekuja ikiwa ni baada ya Bayern kushindwa kuendeleza wimbi lao la ushindi katika ligi kwa kutoa sare ya bao 1-1 na Cologne.
Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, Allianz Arena, Bayern walikuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa Joshua Kimmich, kabla ya Anthony Modeste kuisawazishia Cologne, inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Bundersliga.
“Bado tuna kazi kubwa ya kufanya. Katika kushambulia na hata kulinda, tuna kazi. Tunaweza kuona kuwa hatujafika tunakotaka kwenda,” alisema.