Saturday, January 16, 2021

EUBANK AMTULIZA QUINLAN

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

Bondia Chris Eubank Jr. amemtuliza mpinzani wake, Renold Quinlan, katika raundi ya 10 na kunyakua mkanda wa IBO uzito wa ‘super-middle’.

Eubank alitawala katika pambano hilo la Jumamosi ya wiki iliyopita, huku mpinzani wake kutoka Australia akionyesha wazi kuzidiwa katika pambano hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa London Olympia.

Quinlan alionyesha ukakamavu wa kuendelea na pambano hilo, kwani Eubank alishinda kila raundi kama wengi walivyotarajia.

Kulikuwa na hofu kutoka kwa Quinlan, ambaye alifanikiwa kuvuka raundi ya kwanza baada ya makonde mazito aliyorushiwa.

Hali iliendelea katika raundi ya pili, ingawa Quinlan alijaribu kuwa makini wakati Eubank akitupa makonde yake.

Eubank alimbana mpinzani wake kwenye kamba katika raundi yote ya tatu akimtandika makonde, ingawa Quinlan alijaribu kutoroka kwa kutupia sumbwi moja moja la ‘jab’.

Eubank alionekana kuwa vizuri raundi ya nne, pamoja na raundi ya tano na ya sita, huku Eubank akiendelea kurusha makonde raundi ya saba na nane.

Quinlan alitumia muda mwingi akiwa kwenye kamba wakati Eubank akiendelea kurusha makombora mazito na kibano kwa bondia huyo wa Australia, iliendelea raundi ya 10, kabla ya Howard Foster kuingilia kati.

Naye Andrew Selby alishinda taji la WBC uzito wa ‘fly’ kwa kumchapa Ardin Diale.

Selby, ndugu wa bingwa wa IBF kwa uzito wa ‘feather’ Lee, alishinda raundi zote 10.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -