Thursday, October 29, 2020

FA WATHIBITISHA KUFUNGIA NYOTA WATATU WA MAN CITY

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, England

CHAMA cha Soka cha England (FA), kimethibitisha kwamba wachezaji watatu wa Manchester City, Sergio Aguero, Fernandinho na Nicolas Otamendi kwamba mmoja atatumikia adhabu ya mechi nne, tatu na mwingine moja.

Aguero atafungiwa mechi nne baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Chelsea.

Nyota huyo wa Argentina alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya David Luiz katika mchezo ambao Manchester City walichapwa mabao 3-1 dhidi ya vinara hao wa Ligi Kuu England kwenye Uwanja wa Etihad.

FA uliweka wazi kwenye mtandao wao, wakisema Aguero amepewa adhabu ambayo itamfanya akose mechi dhidi ya Leicester City, Watford, Arsenal na Hull City.

Hii ni mara ya pili kwa Aguero kuadhibiwa msimu huu kwa fujo zake, ambapo alionyeshwa kadi nyekundu dhidi ya West Ham kwa kumpiga kiwiko Winston Reid, Agosti mwaka huu.

Mchezaji mwenzake Fernandinho atafungiwa mechi tatu, baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumsukuma Cesc Fabregas kwenye mabango ya matangazo baada ya kuibuka ugomvi uliosababishwa na faulo ya Aguero.

Naye, Otamendi atafungiwa mechi moja baada ya kuonyeshwa kadi ya njano ya tano msimu huu.

Nyota huyo wa Hispania atakosa mechi ya Jumamosi dhidi ya Leicester.

Kocha Pep Guardiola atakuwa na kazi nzito ama kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake kutokana na kuwakosa wachezaji wake watatu muhimu.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -