Friday, October 30, 2020

FAINALI ZA MABINGWA WA KIKAPU 2017 ZAENDELEA KURINDIMA MWANZA.

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Kufuatia michuano ya mpira wa kikapu iliyozinduliwa na makamu wa raisi Mhe. Samia Suluhu Hassan wiki zilizopita, ameonyesha kuunga mkono zoezi hilo la kuwasaka wawakilishi lililofanyika katika mikoa mbalimbali.

Sprite inaendelea kuibua hisia zaidi ikizileta pamoja zile timu zilizofuzu katika ngazi ya kimkoa kwenye fainali. Michuano ya kinyang’anyiro hiko yalishaanza toka 12 na tayari baadhi ya timu zilishaanza kuchuana huku kila timu ikiwa na matumaini makubwa ya kuibuka bingwa wa kudunda kikapu kitaifa mwaka 2017.

image001

Finali hizi zitaendelea kupigwa mkoani Mwanza ndani ya viwanja vya chuo cha Butimba hadi tarehe 14 huku timu zikicheza mfululizo kwa mtoano ambapo bingwa atapatikana. Maandalizi yakiwa yamepamba moto, timu nazo zinaendelea kujinoa huku wachezaji wakijigamba kuwa mafahali katika finali hizo.

Mshikemshike huu umewazoa mashabiki mbalimbali wa mpira wa kikapu kutoka Mwanza na wengine kutoka mikoa ya jirani kuja kushuhudia. Finali hizi pia zinasindikizwa na burudani za kukata na shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki ambapo msanii Dogo Janja alitokelezea kuchangamsha mshabiki na ‘pafomansi’ la kibabe.

Washiriki wengine wakiwemo wadau wakubwa wa mpira wa kikapu nchini, pia wamejitokeza kushuhudia nani ataibuka kinara.

image002

Lengo kubwa hasa la mashindano haya ni kuibua vipaji vya vijana katika michezo hususani mpira wa kikapu hapa nchini kuanzaia ngazi za chini hadi kitaifa. Na itakuwa ni fursa nzuri kwa vijana kujumuika pamoja na kuleta hamasa kwa vijana wengine kushiriki katika mchezo huu na hatimaye kuibua wachezaji mabingwa kitaifa hata kimataifa.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -