Sunday, November 29, 2020

CANNAVARO AFUNGUKA WATAKAVYOIUA SIMBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

NAHODHA wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amefunga kwamba uzoefu wa wachezaji wake ni sababu tosha ya kuwafunga mahasimu wao Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa Februari 25, mwaka huu, ili waweze kutetea ubingwa wao.

Mwishoni mwa wiki Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United katika Uwanja wa Taifa na kuendelea kujikita kileleni wakiwa na pointi 46, huku mahasimu wao Simba wakiichapa Majimaji 3-0 na kushika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi moja.

Akizungumzia mechi hiyo dhidi ya mahasimu hao, Canavaro alisema wachezaji wa timu yake hawana presha na mtanange huo kwa kuwa wao wanauchukulia kawaida mchezo huo na kuilinganisha Simba na klabu nyingine za kawadia, huku akidaiwa wana uhakika wa kuibuka na ushindi mnono.

“Kwanza nataka ujue kwamba huo ni mchezo wa kawadia, pili wachezaji wetu hawana hofu na mchezo huo kutokana na kwamba wengi wetu wana uzoefu na mechi hiyo, hivyo tumejiandaa kushinda na kutetea taji letu. Simba ndio watakuwa ngazi ya sisi kubeba taji la ubingwa msimu huu,” alisema.

Nyota huyo ambaye pia alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, aliongeza kwamba pamoja na kuuchukulia mchezo huo kama mwingine, lakini pia wamepanga kupambana kufa au kupona kuhakikisha wanabeba pointi hizo dhidi ya Simba na michezo mingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kuwaacha mbali wapinzani wao.

Katika mchezo wa kwanza wa mahasimu hao uliochezwa Oktoba mosi mwaka jana, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Amis Tambwe kabla ya Shiza Kichuya kusawazishia Simba kwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja.

Yanga hawatacheza mchezo mwingine wowote wa Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka watakapomaliza mechi zao mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Ngaya de Mbe ya Comoro, ambapo klabu hiyo ya Yanga mechi ya kwanza wataanzia ugenini Jumapili kisha kurudiana Februari 17, mwaka huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -