Friday, October 30, 2020

FANYA HIVI ILI UMPATE UNAYETAMANI AWE WAKO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

|    NA RAMADHANI MASENGA                 |               


 

NI kweli wapo waliokutana katika daladala na baada ya siku chache wakafunga ndoa na leo wanaishi maisha ya amani na furaha.

Wengine walionana ufukweni na ndani ya wiki kadhaa wakaingia katika ndoa inayowafanya wafurahi na kuwa na amani karibu muda wote. Hayo yanawezekana kutokea.

Unaweza kukutana katika siku chache na mwenzako na kisha baada ya muda kidogo, mkaingia katika uhusiano. Inawezekana. Ila ni moja kati ya kumi!

Wengi waliokutana kwa namna hiyo na kuharakisha kuingia katika uhusiano ni wenye kujuta na kulaumu maamuzi yao. Mapenzi ni suala pana sana.

Si suala linalohitaji papara au uamuzi wa jazba. Kuna misingi na kanuni fulani inabidi kufuata ili uweze kufikia katika uhusiano wa amani, raha na thamani.

Ndiyo, mapenzi ni hisia zinazokuja zenyewe bila kulazimishwa wala kushurutishwa na mtu. Ni hisia zisizochagua mahala pakuonekana wala kujionesha.

Si sahihi kusema eti mpenzi wa kweli nitampata chuoni au kazini, hapana. Wengi walikutana huko wakaambulia maumivu na madhila.

Na wengi walikutana huko wakajikuta wanaingia katika ukurasa wa furaha na amani ya maisha yao. Hakuna eneo wala nchi ya kupata mpenzi wa kweli. Si shuleni, hospitali wala baa.

Kila sehemu ina nafasi yake ya kukupa furaha katika maisha yako na karaha kupitia mapenzi. Suala ni umakini na kufuata misingi bora ya uanzishaji wa uhusiano.

Kuna watu nawajua walikutana sehemu za starehe, sehemu ambazo kwa wengi huamini kuwa si salama kwa kukutania na watu wa maana.

Ila baada ya muda fulani wakaingia katika uhusiano na leo ni miaka kadhaa kuna amani na furaha ndani ya ndoa zao.

Kuna mwanamuziki anaitwa Benjamini alikutana na mpenzi wake katika maandalizi ya video ya wimbo wake.

Alisema alikuwa akitafuta wanawake kwa ajili ya kucheza ndani ya ile video. Alitafuta wasichana wengi ila mmoja wapo alikuwa huyu ambaye leo anamwita mke.

Japo msichana yule hakuwa tayari kwa ajili ya video ile ila baada ya hapo waliwasiliana na matokeo yake imezaliwa ndoa ya furaha na amani kwa mujibu wa maelezo yake.

Suala ninalotaka ulielewe hapa ni kuwa hisia hazina mahala wala muda wa kuonekana. Suala ni umakini na kushusha hali ya haraka katika uanzishaji wa uhusiano wako.

Ndiyo, umekutana na mtu unayeamini unampenda katika daladala ila je, unafuata hatua gani kuingia naye ndani ya uhusiano?

Wengi watachukua namba ya simu leo saa sita mchana, kesho kutwa saa kumi jioni atatongoza. Hapa ndipo wengi tunapoumia na kila siku kulia katika uhusiano.

Anzisha naye urafiki wa karibu usiohusisha mambo ya mapenzi. Tena kuwa mjanja wa kutoonesha kwa pupa hisia zako juu yake ili upate muda wa kumsoma kwa umakini na kumjua jinsi alivyo.

Usiwe na papara, unaweza kuwa naye katika hali hii hata kwa zaidi ya miezi mitatu au minne. Suala si mapenzi ya kweli?

Sasa haraka ya nini? Vijana wengi huwa na pupa ya ngono na matokeo yake wanawahi kutaka kuanzisha uhusiano haraka na kujikuta wakiingia katika majuto na maumivu yasiyokuwa na mfano.

Kuwa makini na kauli na matendo yako katika hali hii. Jitahidi kuwa na ule urafiki utakaokufanya umjue yeye vizuri, marafiki pamoja na nasaba yake.

Hili litakusaidia kumjua vizuri zaidi na kujua yeye hasa ni mtu wa aina gani.

Tunapozungumza kuwa inabidi ujuane na mtu unayetaka kuanzisha naye uhusiano, haina maana ujue jina lake tu  na upate namba yake ya simu. Hapana! Inabidi umjue hasa yeye nani ana mipango gani na mtu wa aina gani.

Ujue tabia yake halisi na hili linawezekana tu kama utamfanya awe rafiki yake huku ile dhamira yako ya kutaka kuanzisha naye uhusiano ukiificha katika hali fulani ili asiweze kuijua na matokeo yake akawa anaonesha tabia za kuigiza.

Instagram:ramadhan.masenga

Mwandishi wa makala hii ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa uhusiano, maisha na utulivu wa hisia( Psychoanalyst)

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -