Tuesday, October 20, 2020

FANYA HIVI UNAPOHISI UNASALITIWA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

KATI ya wengi wanaosoma makala hii, baadhi yao wana wasiwasi na wapenzi wao. Hawaamini kabisa kama mahusiano yao yapo salama. Hawaamini kama ni wao tu ndiyo wapo katika mioyo ya wandani wao.

Wanahisi kuna kitu kinajipenyeza katika mahusiano yao ambacho kitaharibu furaha na amani ya nafsi zao. Baadhi mko hivyo katika mahusiano yenu. Hakuna hata chembe za utulivu katika mioyo yenu

Nafsi zenu hazina amani linapokuja suala la kufikiria mahusiano.Neno usaliti linapita kila dakika katika ubongo wenu kama namna ya redio inavyozungusha kanda. Usaliti ni kitu ambacho hakiwezi kuvumilika. Nani anaweza? Usaliti kitu kingine bwana!

Nani anaweza kuona kipenzi chake cha nafsi kikimsaliti na kisha kuchukulia kawaida tu. Nani? Hakuna.

Mara nyingi hali kama hiyo inapotokea mahusiano ndiyo yanakuwa yamefikia tamati. Wakati mwingine huwa haijalishi ni visingizio gani vitatolewa. Mchezo unakuwa umefika tamati.

Wengi wanaamini hakuna msaliti wa mara moja. Huamini msaliti akianza leo basi kila siku atakuwa anafanya hivyo. Siwezi kuongea sana katika hili kwa sababu hii ni mada nyingine kwa siku nyingine.

Nikumbushe tu, lengo la mada hii kama kawaida ni kwa wale walio katika mahusiano ya kweli na yenye malengo chanya.Si kwa wale ambao karibu kila mwisho wa mwezi wana wapenzi wapya. Hapana!

Japo ni ukweli usiopingika kwamba usaliti hauvumiliki, lakini ni vyema ukawa na uhakika kwamba mpenzi wako anakusaliti kweli.

Katika hili, katu usiache kujiamini na wala usiruhusu wasiwasi uhusike. Maana wengi waliongozwa na fikra zao bila kuwa na uhakika na kujikuta wakitoa maamuzi yasiyo sahihi. Wamewaacha wapenzi wao kwa tuhuma zisizo za kweli.

Wengi huwa na wasiwasi kuwa wanasalitiwa na wenza wao, eti kwa kuwa wanachelewa kurudi, kuchelewa kupokelewa simu zao na kadhalika. Si mbaya kuwa na umakini kwa matendo ya mpenzi wako, ila pia haifai kuwa na wasiwasi katika sababu dhaifu kama hizi bila kujua kwa undani sababu za yeye kufanya hivyo.

Eti kweli kuchelewa kurudi nyumbani itoshe kuwa sababu ya kuamini unasalitiwa? Nani asiyejua tabu ya usafiri katika Jiji hili? Nani asiyejua katika baadhi ya maeneo Tanzania usafiri ni shida sana kupatikana? Hapana sababu hii haitoshi.

Mpenzi wako pia anaweza kuchelewa kupokea simu kutokana na sababu nyingine tu, si eti yuko na hawara.

Kwani unafikiri anashindwa kuwa na hawara na kumwambia kuwa yeye ni mke au mume wa mtu? Akimwambia hivyo na mhusika kuelewa, unadhani atashindwa kupokea simu mbele yake. Na hii pia si sababu ya maana sana.

Ili uweze kufurahia mahusiano yako, inabidi ujiamini na kujikubali na si kuyumbishwa na fikra dhaifu kama hizi.

Na ili uweze kujiamini zaidi ndiyo maana unatakiwa kuingia katika mahusiano na mtu ambaye una uhakika anakupenda kwa dhati na si kuwa anakupendea kitu. Katika mahusiano na mtu wa aina hii, amani katika moyo ni jambo la uhakika kabisa. Kiujumla wasiwasi wa kusalitiwa huwa unaanza hapa.

Pale unapoanza kuziona baadhi ya tabia mpya kwa mpenzi wako hasa zile zisizo kufurahisha. Kama anapoanza kuwa muongo, anapopunguza kukupigia simu kama ilivyokuwa mwanzo, anapoanza ukali usio na sababu unapotaka kushika simu yake.Kukuficha kuona pale anapokuwa anachati katika mitandao ya kijamii na mambo mengine mengi ya kukutia wasiwasi.Ila katika hatua kama hii, pia japo inaashiria usaliti hautakiwi kuwa na pupa.

Kuwa mstaarabu zaidi huku ukifanya upelelezi wa kimya kimya ili uweze kupata ukweli halisi. Baada ya kupata ushahidi wa kutosha juu ya wasiwasi wako kwa mhusika. Mueleze ukweli huku ukitoa ushahidi wa suala zima.

Epuka kuwa na munkari katika kipindi hicho chote. Akitaka kutoa utetezi kwa kile alichofanya, unaweza kumruhusu.

Lengo la kuusikiliza utetezi wake si kuonesha moja kwa moja hali ya kumsamehe.Hapana, bali kutaka kujua kama chanzo ulikuwa wewe au yeye ili kama tatizo ni wewe, ujue huenda kumwacha ikawa si suluhisho maana kuna hatari hata mwingine pia anaweza kukusaliti.

Ila pia katika upande mwingine kama ukigundua hakuwa anakusaliti, unatakiwa kujua huenda ukawa na tatizo.

Huenda ukawa una wasiwasi ambao kimsingi ni ugonjwa kisaikolojia. Na kama una ugonjwa huu basi jua katu huwezi kujiamini na matokeo yake unaweza kujikuta kila siku unaacha wapenzi kwa kuwapa tuhuma ambazo si sahihi kwao.

Kama yalivyo maradhi mengine, huu pia una tiba yake. Cha kufanya ni kwenda kwa mwanasaikolojia kupata tiba ili uweze kupata ahueni ya nafsi yako na hatimaye uweze kufurahia maisha yako ya kimahusiano.Itoshe hapa kwa leo.

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -