Friday, October 30, 2020

Faraja Kotta akumbuka kidonda cha Miss kilivyomtesa

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA,

MISS Tanzania 2004, Faraja Kotta, ametoka mafichoni na kukumbuka maumivu aliyopata baada ya wadau mbalimbali kuponda ushindi wake alioupata.

Faraja aliyezaliwa Mei 6, mwaka 1985, amekumbuka mateso hayo baada ya Miss Tanzania 2016, Diana Edward, kuanza kushutumiwa kwa kashfa mbalimbali kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kutokana na tuhuma hizo za Miss Tanzania 2014, Faraja amesema kuwa anakumbuka kejeli alizopata baada ya ushindi wake huo ulivyomwathiri.

“Niliposhinda Miss Tanzania, kuna mtangazaji fulani alitumia kama saa zima hewani kusema ambavyo sikustahili kushinda, nilitetemeka, nilishindwa kuoga, kula; nilijifungia ndani siku nzima nikilia. Niliwaza sana ambavyo pengine ni kweli sikustahili. Nilijuta kushiriki Miss Tanzania.

“Nilikuwa mdogo nikiwa na miaka 19 tu nikiwa nimetoka ‘boarding school’ (shule ya bweni), sikujua kuna watu wanaweza kuwa na roho mbaya hata kwa watu wasiowajua, nilimwambia baba (aliyetangulia mbele za haki) na kila busara waliyonayo kunifanya nijisikie vizuri.

Alimaliza kwa kusema: “Kuna sehemu ya nguvu niliyonayo leo iliyotokana na kujeruhiwa na binadamu na kupona. Lakini si kila mtu atapata bahati ya kupona, unaweza kumjeruhi mtu na akapotea moja kwa moja. Usijitafutie laana za reja reja tujenge zaidi ya kubomoa.”

Ujumbe huo wa Faraja umewafanya mashabiki wake kumpongeza kwa ujasiri aliouonyesha wa kutokata tamaa baada ya wadau hao kuponda uhalali wake wa ushindi huo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -