Wednesday, October 28, 2020

Azam FC: Farid Mussa sasa anajuta

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA,

UNATAKA kusikia kitu gani kuhusu Farid Mussa? Yule winga aliyekuwa chachu ya Azam, Kombe la Kagame mwaka jana? Hivi unajua kama bado tupo naye kitaa tunapiga naye stori tu.

Farid ambaye alikuwa gumzo kwenye michuano ya Kagame iliyofanyika pale Taifa na Azam kutwaa ubingwa mpaka sasa bado yupo Dar es Salaam tunapigana naye vikumbo kama kawaida.

Winga huyo wa kushoto mwenye kasi, uwezo wa kumiliki mpira, kupiga chenga, kukokota mipira na akili na maarifa amekwama safari yake ya kusakata kabumbu nje ya nchi.

Ilielezwa amefuzu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Hispania takribani miezi nane iliyopita, lakini hadi sasa hajaenda licha ya kwamba timu yake ya Azam ilimwondoa kwenye usajili wake wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

Kukwama kwake na kuendelea kusota kumelifanya BINGWA kumtafuta na kuichambua kwa kina safari yake hiyo ya kuhakikisha anacheza soka la kimataifa.

Afunguka mazito

Kwa masikitiko makubwa, Farid amefunguka na kutaja kile kinachomkwamisha kutimka nchini kwenye klabu yake mpya ya Deportivo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza huko Hispania.

“Bado nipo nchini, ninasubiri visa ubalozi wa Hispania wa hapa, kwa kweli imekuwa muda mrefu sana sasa hadi nashindwa kuelewa nini kinasababisha,” alisema Mussa.

Mbali na visa, Farid alisema kibali cha kazi pia kimekuwa tatizo kubwa ambalo limemfanya kuendelea kusota nchini mpaka sasa na kushindwa kutimiza ndoto zake.

“Mbali na visa pia sina kibali cha kazi ambacho kitaniwezesha kuishi nchini Hispania ambapo bado mpaka sasa sijajua nakipata lini ili niweze kwenda,” alisema.

Alisema kuwa ukweli wa sakata la safari yake utajulikana mwishoni mwa wiki hii kama ataondoka au asubiri dirisha dogo ili aweze kuendeleza kipaji chake.

“Sakata langu hadi mwishoni mwa wiki hii nitajua mbivu na mbichi, kama safari ipo au ndio nisubiri ligi ya Bongo kwenye dirisha dogo la usajili litapofunguliwa,” alisema.

Safari yake 50-50

Farid aliyewahi kuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichoivaa Nigeria, alikuwa kati ya wachezaji wanne waliokuwa mbele kusukuma mashambulizi katikati na pembeni amesema kuwa safari yake ipo 50 kwa 50 mpaka sasa.

Alisema ukiacha visa na kibali cha kuishi pia kuna nyaraka ambazo Azam wanapaswa kuzituma nchini Hispania ili aweze kutimiza malengo yake.

“Mpaka sasa nasema safari yangu ipo fifty-fifty kwa sababu kuna mambo mengi sana ambayo bado hata nikipata visa leo kibali cha kazi sina naendaje, hivyo sijui,” alisema.

Ajuta jina lake kutokuwemo Azam

Kitendo cha kufuzu majaribio na Azam kukubali kumtoa kwa mkopo wa miaka miwili kwenye klabu hiyo, wanalambalamba hao walimwondoa kwenye mipango yao ya msimu huu.

Sababu kubwa ambayo Azam waliitaja ni kuwa tayari staa huyo hatakuwemo kwenye mipango ya timu hiyo kutokana na ukweli kuwa walishamtoa kwa mkopo na muda wowote ataondoka nchini.

Akizungumzia kutokuwemo kwa jina lake kwenye majina ya wachezaji 27 yaliyotumwa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alisema ni kitu anachojuta mpaka leo.

“Kwa kweli najuta jina langu kutokuwemo kwenye usajili msimu huu, nina imani hata Azam nao wanajuta, kwani ningeweza kuonekana kwenye ligi ya Bongo ila sasa nimebaki nafanya mazoezi tu,” alisema.

Aendelea kujifua kivyake

Farid mwenyewe amesema amekuwa akifanya mazoezi ya peke yake tu kwa miezi miwili sasa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

“Nipo naendelea na mazoezi ili niendeleze kipaji changu na kama safari ikigoma basi nitasajiliwa dirisha dogo ili nicheze Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema.

Azam wanena

Mabosi wa Azam wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawembwa, walisema safari ya winga huyo imekwama kutokana na sababu kadhaa ila kwa sasa kila kitu tayari ila kinachosubiriwa ni kibali cha kazi tu.

“Tunasubiri kibali cha kazi tu kwa sasa kwani kila kitu tayari na muda wowote anaweza kuondoka na kwenda kuendeleza kibaji chake alichokuwa nacho,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -