Thursday, November 26, 2020

FEBRUARI 18 ITAKUWAJE KWA LWANDAMINA?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ONESMO KAPINGA

BAADA ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyofanyika visiwani Zanzibar na Azam kutwaa ubingwa baada ya kuifunga bao 1-0 Simba, sasa timu za Bara zimerejea jijini Dar es Salaam kuendelea na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ligi hiyo itaendelea leo kwa timu ya Toto Africans itakapocheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, lakini kesho kutwa kukiwa na mechi tatu kati ya Majimaji na Yanga, wakati Simba watakuwa Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar huku Azam wakiwakaribisha Mbeya City.

Yanga watakuwa na kibarua kizito cha kuhakikisha wanaibuka na ushindi ili kupoza machungu ya mashabiki wao baada ya kufungwa mabao 4-0 na Azam katika mchezo wa makundi wa Kombe la Mapinduzi.

Kipigo kingine cha changamoto ya mikwaju ya panelti 4-2 kufuatia sare tasa katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, walichokipata kutoka kwa watani wao wa jadi Simba ni moja ya sababu nyingine ambayo itawafanya Yanga kupigania pointi tatu dhidi ya Majimaji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Lakini Yanga wenye pointi 40 wanahitaji ushindi wa hali na mali ili wasiendelee kuacha tofauti ya pointi nyingi dhidi ya Simba ambao wanaongoza ligi hiyo kutokana na pointi 44.

Kwa upande wa Simba, nao watataka kuwapa furaha mashabiki wao baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi iliyochezwa Ijumaa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.

Licha ya Simba kufungwa na Azam, lakini kocha mkuu wa Yanga, George Lwandamina, anaonekana kuwa na mtihani mkubwa kutokana na rekodi aliyoanza nayo katika kikosi hicho.

Rekodi ya Lwandamina imekaa vibaya kama anataka kuifikia ile ya kocha aliyemtangulia Hans van der Pluijm, ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.

Katika mechi kadhaa alizoziongoza zikiwamo za kirafiki, michuano ya Kombe la Mapinduzi na Ligi Kuu Bara, inaonyesha dhahiri kwamba bado hana kazi kubwa ya kufikia rekodi ya Pluijm.

Ukiangalia Pluijm ameiongoza Yanga katika mechi 83 kabla ya kuvuliwa wadhifa wake na kukabidhiwa cheo kipya, ambacho hakikuwapo kwa muda mrefu katika klabu hiyo.

Katika mechi hizo, Pluijm walishinda  mara 51 sawa na pointi 170, ambapo walitoka sare mara 17 na kupoteza mechi 15 ikiwamo ile ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa  na Kombe la Shirikisho barani  Afrika.

Lwandamina hadi sasa ameiongoza Yanga katika mechi nane ikiwamo Ligi Kuu ya kirafiki na ile ya Mapinduzi na ukilinganisha na nane za awali ya Pluijm, inaonyesha yeye alikuwa juu yake.

Katika mechi hizo nane za awali za Pluijm alishinda tano sare tatu akiwa hajapoteza, huku timu ikifungwa mabao 24 na kufungwa matano, wakati Lwandamina yeye alishinda mechi nne, amepoteza mmoja sare mitatu sawa na pointi 13 huku timu ikiwa imefunga mabao 16 na kufungwa saba.

Pluijm alianza kwa sare tasa dhidi ya KS Flamurtari Vlore na pia sare ya  mabao 2-2 dhidi ya Simurg PIK, walipokuwa kambini Uturuki, aliifunga Ashanti United 2-1, Coastal Union 0-0, Mbeya City wakashinda tena 1-0, mechi ya Ligi Kuu Bara.

Katika michuano ya kimataifa aliongoza Yanga kuifunga Komorozine mabao 7-0 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kabla ya kuifunga mabao 5-2 katika mechi ya marudiano ugenini Ligi ya Mabingwa Afrika na baadaye kukamilisha mechi ya nane kwa kuichapa mabao 7-0 Ruvu ya Ligi Kuu Bara.

Lwandamina alikaribishwa kwa kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa JKU ya Zanzibar katika mechi ya kirafiki, alishinda mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu na sare ya bao 1-1 dhidi ya African Lyon, kabla ya kushinda mabao 4-0 dhidi ya Ndanda FC ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Bara.

Yanga ikiwa chini ya Lwandamina kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, ilianza kwa ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Jamhuri ya Pemba,  kisha ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zimamoto, baadaye alifungwa mabao 4-0 na Azam FC na kufungwa na Simba kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-2.

Matokeo hayo hayakuwa mazuri kwa mashabiki wa Yanga, licha ya kwamba katika mechi hiyo wachezaji wao walionyesha kiwango wa hali ya juu.

Februari 18 mwaka huu, timu hizo zitakutana kwa mara nyingine katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara, kwenye Uwanja wa Taifa, lakini siku hiyo itakuwaje kwa Lwandamina, ukizingatia Pluijm alitoa sare ya bao 1-1.

Tukutane Jumatatu ijayo

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -