Friday, October 30, 2020

FEISAL KURUDISHA MABAO YA MZIBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

KIUNGO  mkabaji wa timu ya Yanga, Feisal Salum Abdalla ‘Fei Toto’, amesema anatarajia kuja kivingine, akijiandaa kufunga mabao kwa kichwa Ligi Kuu Tanzania Bara ikirejea Juni 13, mwaka huu.

Wachezaji wa Yanga waliokuwa na uwezo wa kufunga mabao  ni Abeid Mziba, Said Mwamba ‘ Kizota’, Omar Hussein na Mzambia  Davis Mwape.

Akizungumza na BINGWA jana, Fei Toto alisema licha ya nafasi anacheza ya kiungo mkabaji, lakini anataka kuwasaidia mshambuliaji wa timu hiyo kufunga mabao ya kichwa.

 Fei Toto ambaye alifanikiwa kufunga  bao la pili kati ya mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar es Salaam, alisema kazi imeanza kuelekea michezo iliyosalia ya ligi hiyo.

Katika mchezo huo, Fei Toto alifunga bao lake baada ya kupokea krosi kutoka kwa Juma Abdul, lingine lingine likifungwa na Bernard Morrison kwa mkwaju wa penalti na Mrisho Ngassa  aliyemalizia pasi ya Gnamain Yikpe.

Akizungumza na BINGWA jana, Fei Toto  alisema wakati ligi iliposimama kutokana na hofu ya virusi vya corona, alijiongeza  kufanya mazoezi  ya kufunga mabao ya kichwa.

“Pamoja na nilikuwa nafanya  mazoezi kutokana na programu nilizopewa na kocha, lakini mwenyewe nilikuwa nafanya mazoezi ya kufunga mabao kwa kichwa, lengo langu ni kuwa na uwezo wa kuipa timu mabao katika aina yoyote  ya ufungaji,”

“Nataka kuwa na uwezo wa kufunga kwa miguu yote na kutumia kichwa kwa sababu kuna wakati mipira inakujia kwa juu halafu unakuwa hauna mazoea ya kupiga kwa vichwa,” alisema Fei Toto.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -