Wednesday, November 25, 2020

‘First Eleven’ ya wanaowania Ballon d’Or mwaka huu

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

SIKU chache zilizopita orodha ya mastaa 30 wanaowania tuzo ya Ballon d’Or iliwekwa hadharani.

Wengi wametabiri kuwa huenda Cristiano Ronaldo akanyakua tuzo yake ya nne.

Wanaamini kuwa licha ya Ronaldo kuanza vibaya msimu huu, nyota huyo anajivunia mafanikio yake ya kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na lile la Euro 2016.

Kwa tawimu zake za mwaka huu, amepachika jumla ya mabao 41 akiwa na Madrid na timu yake ya Taifa ya Ureno.

Lakini mbali na Ronaldo, kuna mastaa wengine wanaoitolea jicho tuzo hiyo.

Messi aliiwezesha Barcelona kuchukua ubingwa wa La Liga na amepachika mabao mengi (49) kuliko Ronaldo.

Ukiachana na hao, orodha hiyo inawajumuisha pia Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, Luis Suarez, Neymar na Gareth Bale.

Tangu mwaka 2008, tuzo hiyo haijanyakuliwa na mchezaji mwingine zaidi ya Messi na Ronaldo.

Makala haya yanakuletea kikosi cha kwanza ‘First eleven’ inayotokana na orodha hiyo wa wachezaji 30.

Kipa: Manuel Neuer (Bayern Munich)

Neuer alithibitisha kuwa ni mmoja wa walinda mlango hatari duniani mwaka 2016.

Aliiongoza Bayern kunyakua taji la Bundesliga na aliiwezesha timu ya Taifa ya Ujerumani kufika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro 2016.

Bila shaka anastahili kusimama langoni katika kikosi hiki cha mastaa wa Ballon d’Or.

Beki wa kulia: Sergio Ramos (Real Madrid)

Ramos si beki wa kulia lakini anacheza nafasi hiyo katika kikosi hiki kutokana na uhaba wa walinzi katika listi hiyo ya wachezaji 30 wanaoipigania tuzo ya Ballon d’Or.

Ramos alikuwa nahodha wakati Madrid ilipochukua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mchezo wa fainali dhidi ya Atletico, Mhispania huyo alifunga bao la utangulizi.

Pia alifunga bao katika changamoto ya mikwaju ya penalti.

Beki wa kati: Diego Godin (Atletico Madrid)

Ni wazi kuwa Godin ni mmoja kati ya mabeki wazuri wasiozungumziwa sana barani Ulaya.

Staa huyo raia wa Uruguay amekuwa nguzo imara ya safu ya ulinzi ya Atletico tangu mwaka 2010.

Godin aliiongoza timu hiyo kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa wafuatiliaji wa La Liga, hawawezi kushangaa kuona jina la staa huyo likiingia kwenye first eleven hii.

Beki wa kati: Pepe (Real Madrid)

Pepe amekuwa haeleweki anapokuwa uwanjani na hilo linatokana na aina ya uchezaji wake wa kibabe.

Mwaka huu ulikuwa mtamu kwake kwani baada ya kuipa Madrid Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, alitwaa lile la Euro 2016 akiwa na Ureno.

Kutokana na mafanikio hayo, ni ngumu kumnyima namba kwenye kikosi hiki na ikizingatiwa kuwa ni mmoja kati ya mabeki watatu tu waliopo kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaoiwania Ballon d’Or.

Beki wa kushoto: Gareth Bale (Real Madrid)

Bale anaweza kuitendea haki nafasi hii ikizingatiwa kuwa hakuna beki wa kushoto kwenye orodha hiyo ya wachezaji 30.

Ikumbukwe kuwa Bale aliicheza kwa ustadi wa juu nafasi hiyo alipokuwa na wakali wa Kaskazini mwa London, Tottenham.

Mwaka huu alinyakua kwa mara ya pili taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Madrid.

Akaiwezesha Wales kutinga hatua ya nusu fainali ya Euro 2016 kwa mara ya kwanza katika historia ya soka nchini humo.

Katika mashindano hayo yaliyofanyika Ufaransa wakati wa majira ya kiangazi, nyota huyo alipachika mabao.

Kiungo wa kati: Andres Iniesta (Barcelona)

Ana umri wa miaka 32 lakini kazi zake ni zaidi ya chipukizi wa miaka 16 au chini ya hapo.

Bado Iniesta ni mmoja kati ya viungo bora Hispania na Ulaya.

Msimu uliopita, alishinda taji lake la nane la La Liga akiwa na Barca.

Alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Hispania katika michuano ya Euro 2016 ingawa haikufanya vizuri.

Kiungo wa kati: Luka Modric (Real Madrid)

Nani aiyekunwa na aina ya uchezaji ya Luka Modric? Bila shaka hakuna.

Kiungo huyo raia wa Croatia ana umri wa miaka 31 lakini bado ameonesha kuwa silaha ya safu ya kiungo ya Madrid.

Hakuna atakayebisha kuwa Modric alistahili kuwa kwenye kikosi hiki na kukabidhiwa ‘dimba’ lake.

Kiungo wa kati: Toni Kroos (Real Madrid)

Licha ya Kroos kuwa na umri mdogo wa miaka 26, ameonesha kuwa anastahili kuichezea Madrid.

Baada ya kushinda mataji matatu ya Bundersliga akiwa na Bayern, Mjerumani huyo anaweza kufanya hivyo akiwa na Madrid.

Kwa misimu miwili aliyokaa Bernabeu, nyota huyo amekosa mechi nane pekee.

Straika: Lionel Messi (Barcelona)

Kuna uwezekano mdogo kwa Messi kuchukua tuzo ya mwaka huu.

Msimu uliopita alifunga mabao 41 katika mechi 49 alizoichezea Barca.

Kwa mabao hayo, aliiwezesha timu hiyo kuchukua La Liga na Copa del Rey.

Akaipeleka Argentina fainali ya michuano ya Copa America kabla ya kukosa penalti katika mchezo wa mwisho ambao ungewapa ubingwa.

Straika: Cristiano Ronaldo (Real Madrid)

Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kumpiku Messi na kushinda tuzo hiyo.

Alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya na kasha kuipa Ureno taji la Euro 2016.

Straika: Luis Suarez (Barcelona)

Katika orodha ya wachezaji hao 30, mbali na Suarez, washambuliaji wengine waliokuwemo ni Griezmann na Neymar, lakini ni Mruguay huyo ndiye aliyepata bahati ya kuingia kwenye kikosi hiki.

Msimu uliopita aliziona nyavu mara 59 na amethibitisha kuwa ni moto wa kuotea mbali katika kuwatesa walinda mlango.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -