Wednesday, October 28, 2020

FLAVIANA ALIVYOWAFUNDA WAREMBESHAJI KUCHA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HERIETH FAUSTINE


MWANAMITINDO wa Kimataifa, Flavian Matata, ni moja kati ya walimbwende ambao wamekuwa wakiendelea kufanya vyema kwenye fani hiyo.

Pamoja na mafanikio yake kwenye fani ya mitindo, pia amejitanua vyema katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kijamii na ujasiriamali.

Baada ya kufanya vizuri kwenye masuala ya kijamii, kwenye upande wa ujasiriamali mwanamitindo huyo ameendelea kutoa fursa kwa vijana kujiajiri kupitia fani ya urembo baada ya kuzindua rangi za kucha ambazo zimeonekana kupendwa sana na wanawake.

Kupitia Kampuni yake ya urembo iitwayo Lavy Nail Polish, Flaviana ametoa mafunzo kwa vijana wanaofanya biashara ya kupaka rangi za kucha mitaani na kuwataka wasikate tamaa na fani hiyo.

Licha ya kudharauliwa kwa fani hiyo na kuonekana inafanywa na watu waliokosa kazi za maana, lakini Flaviana anasema kazi hiyo ni moja ya kazi muhimu sana katika fani ya urembo.

Katika mafunzo yaliyaondaliwa na Kampuni ya Lavy Nail Polish na kufunguliwa  na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamisi Kigwangala, alisema kupitia juhudi zinazofanywa na kampuni hiyo katika kuwainua vijana wasio katika sekta rasmi, Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi hizo ili kuleta maendeleo.

Alisema Serikali inatambua kuwa ujasiriamali ni fursa muhimu kwa vijana kujiajiri, hivyo haina budi kuunga mkono juhudi hizo.

“Nchi hii ni miongoni mwa nchi zinazoendelea na imepata nafasi kubwa ya kupata michango kutoka kwa vijana hasa wa kike na wa kiume.

“Shughuli zisizo rasmi zimechangia kupunguza pengo la wasio na kazi kwa kutoa fursa kwa vijana kupata shughuli mbalimbali za kujipatia kipato.

“Fani ya urembo wa kucha si ya kudharauliwa kutokana na kuwa na kipato kikubwa, nawasihi vijana wajiunge katika mafunzo ya kucha ili kujipatia ajira na kujiajiri,” alisema Kigwangala.

Alisema mafunzo hayo yaliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwaongezea ujuzi vijana katika eneo la utengenezaji wa kucha salama kwa kuzingatia usafi binafsi na wa mazingira.

Alisema kutokana na biashara hiyo kufanywa na wanaume, aliwataka na wanawake kujitokeza na kuchangamkia fursa hiyo.

“Naunga mkono jitihada zinazofanywa na Flaviana kwa ubunifu mkubwa  alioufanya na kuamua kuuleta nyumbani,” alisema.

Akisoma risala kwa niaba ya watengeneza kucha nchini, Mark Msekwa, alisema ujuzi wa utengenezaji kucha  ulianza kukua kwa kasi kuanzia mwaka 1990 na kusababisha saluni nyingi kufunguliwa na kuwepo kwa ongezeko kubwa la vijana kufanya kazi hiyo kwa kuajiriwa au kujiajiri.

Alisema kwa sasa wastani wa kipato cha mtengeneza kucha ni kati ya Sh 200,000 na zaidi ya Sh milioni moja kwa mwezi na kulingana na mahali mtu anapofanyia kazi.

“Kwa kipato hiki, tumekuwa tukimudu maisha yetu kwa kulea familia, kusomesha watoto na wakati mwingine kufanya kazi za kujitolea katika jamii.

Pamoja na mafanikio makubwa tunayoyapata, bado taaluma hii ina changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma hamasa za vijana wengi kujiunga na kazi hii.

“Alisema changamoto ya kwanza ni jinsi jamii inavyoiona kazi hiyo kuwa ni kazi zinazofanywa na watu walioshindwa maisha kuonekana hawana kazi nyingine ya kufanya na kufanya vijana wengi kuionea haya.

“Changamoto ya pili ni kutotazamwa na Serikali kama eneo la ajira inayoweza kuchangia pato kwa wananchi kwa kiwango kikubwa.

Naye Flaviana Matata, alisema yeye pamoja na Kampuni yake wataendelea kutoa mafunzo kwa vijana hao ili kuwaongezea utaalamu lakini pia kuiongezea thamani kazi hiyo.

“Watengeneza kucha lazima wawe na ujuzi lakini pia watumie bidhaa zilizo bora katika kazi zao, kumekuwa na wimbi kubwa la wanawake kuharibika kucha zao, hii inatokana na ukweli kwamba watengeneza kucha wanatumia bidhaa zisizokuwa na ubora, hivyo tunatoa mafunzo sambamba na kuwataka kutumia bidhaa zetu bora zenye viwango vya kimataifa,” anasema Flaviana.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -