Friday, November 27, 2020

FLOYD MAYWEATHER BIBI YAKE NDIYE SIRI YA UTAJIRI ALIONAO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LOS ANGELES, Marekani

BAADA ya kuwa kwenye ulimwengu wa masumbwi kwa kipindi cha miaka 20 sasa, bondia Floyd  Mayweather amejijengea heshima kubwa katika mchezo huo na anatajwa kuwa na wafuasi wapatao milioni 30.5 katika akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Safari yake katika kufikia mafanikio hayo haikuwa nyepesi hata kidogo na mara nyingi amekuwa akiizungumzia, lengo likiwa ni kuwatia moyo binadamu wengine wanaohisi changamoto ni adhabu kwao.

“Haikuwa rahisi (kuwa tajiri). Nilikulia katika maisha magumu sana. Nilizaliwa Michigan. Baba yangu alikuwa bondia na kaka zangu wawili walifanya kazi hiyo pia. Kila siku baba yangu alinichukua na kunipeleka ‘gym’,” alisema Mayweather na kuongeza:  “Ilikuwa ni safari ndefu.”

Hata hivyo, baba yake hakuwa akitegemea masumbwi pekee, kwani hakuwa akipata kipato cha kukidhi mahitaji ya familia. “(Baba) alikuwa mpambanaji, alijiingiza katika mishe za mtaani. Aliwahi kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani,” alisema Floyd.

Baba huyo aliwahi kusema wazi kuwa alikuwa akijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya ili kuinua kipato cha familia yake. “(Floyd) alikuwa akinufaika na dawa nilizokuwa nikiuza. Alikuwa akipata chakula cha kutosha. Alikuwa akivaa nguo nzuri, na nilikuwa nikimpa fedha. Hakuwa na shida. Kama si mimi, huenda leo hii asingekuwa hapo alipofika.”

Floyd amewahi kukiri kuwa, hakuwa akishangaa kurudi nyumbani na kukuta sindano za dawa za kulevya zikizagaa ndani, kwani mama yake alikuwa mtumiaji na hata shangazi alifariki kwa Ukimwi kutokana na dawa hizo.

“Watu wanapoona mafanikio yangu ya sasa, huwa wanashangaa, kwani sikuzaliwa na kukuta chochote.”

Floyd aliongeza kuwa, baba yake aliwahi kulazwa hospitalini kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kupigwa risasi na kaka wa mama yake, jambo lililoongeza hali mbaya ya kiuchumi kwenye familia yao.

“Madaktari waliniambia baba asingewezea kutembea tena. Hata hivyo, alipona na kuanza kupanda ulingoni.  Alikuwa moto wa kuotea mbali, lakini hakupata nafasi ya kupigania ubingwa wa dunia.”

Akiwa kwenye familia iliyotawaliwa na umasikini, bibi yake ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kugundua kipaji cha Floyd, ambaye kwa sasa anatajwa kuwa na utajiri wa kiasi cha Dola za Marekani milioni 600 (zaidi ya Sh trilioni 1.3).

Baada ya kufukuzwa shule, bondia huyo alimwambia bibi yake anatafuta kazi ya kufanya na ndipo kikongwe huyo alipomwambia: “Hapana, endelea kucheza masumbwi.”

Kutokana na hali ngumu ya kimaisha, familia ya watu saba ya Floyd iliishi kwenye chumba kimoja na kuna kipindi hata fedha za kununua umeme ziliwashinda.

Floyd aliongeza kuwa, alipoingia rasmi kwenye ndondi alikuwa na ndoto za kufika Uingereza kudundana na mabondia wakubwa, jambo ambalo baadaye lilitimia.

Mayweather alitoa historia yake hiyo ya maisha ya mateso aliyopitia kuelekea pambano lake na Conor McGregor, ingawa kuna taarifa kuwa huenda lisifanyike kama ilivyotangazwa hapo awali.

Ikiwa mabondia hao watakubaliana kupanda ulingoni na kudundana, pambano lao litazalisha kiasi cha Dola za Marekani milioni 300.

“McGregor ana mabosi wake. Mimi sina mabosi. Kama Conor McGregor anataka kupigana na mimi, basi tunaweza kufanya hivyo.

“Katika pambano moja, natengeneza kiasi cha fedha ambacho Conor McGregor amekipata kwa kipindi chote alichocheza masumbwi,” anasema.

Kinachosubiriwa kwa  hamu kwa sasa ni kufanyika pambano hilo, kwani litamfanya Mayweather kuwa mwanamasumbwi aliyeingiza fedha nyingi kuliko wote duniani.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -