Saturday, November 28, 2020

FORLIE KACHA, MSANII WA TANZANIA ALIYEWAKOSHA MARAIS AFRIKA KUSINI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

KATIKA siku za hivi karibuni tumeendelea kushuhudia sanaa yetu ikipiga hatua na kufanikiwa kuwateka mashabiki wengi siyo wa ndani pekee bali hata wale waliopo nje ya nchini yetu.

Juhudi binafsi za wasanii na wadau wa sanaa zimepelekea Tanzania iwe nafasi za juu kabisa miongoni mwa nchi za Afrika zinazofanya vizuri kwenye sanaa hasa ile  ya muziki huku filamu nayo ikijikongoja.

Inawezekana kwenye filamu kuna vipaji vingi na vinafanya vizuri ila kasi ya Bongo Fleva inafanya wasanii hawa wachache wanaofanya vyema kwenye filamu wasionekane. BINGWA leo lipo na mmoja ya wasanii aliyetembea nchi nyingi kuitangaza sanaa ya Tanzania na kukuza jina lake.Huyu si mwingine bali ni Fortunatus  Kasomfi ’Forlie Kacha’.

FORLIE KACHA NI NANI HASA

Huyu ni msanii wa mwenye vipaji lukuki vikiwemo,kucheza ngoma za asili, sarakasi, mchongaji, Mtangazaji na mwimbaji.

Pia ni mahiri katika kuicheza  Mpira wa Kikapu, Wavu na soka.

“Nimesoma Shule ya Msingi Sisimba iliyopo Mbeya, nilipomaliza nikaenda Mbeya Sekondari na nikachanguliwa kusoma kidato cha tano mpaka cha sita katika Shule ya Tosamaganga, Iringa.Chuo nimesoma Johannesburg Institutes of Technology Gandhi Joburg Afrika Kusini,” anasema.

AWEKA ELIMU PEMBENI ELIMU

Forlie Kacha anasema baada ya kumaliza masomo yake ya Chuo Kikuu huko Afrika Kusini aliona ni muda mwafaka wa kufanya kile alichokuwa anakitamani muda mrefu, sanaa ndiyo ilikuwa kiu yake kubwa na hapo ndipo alipoanza kujichanganya kwenye majiji mbalimbali Afrika Kusini.

Baada ya kumaliza chuo nikaanza kutafuta nafasi nzuri ya kufanya sanaa, nilikuwa msanii wa sauti (Voice over artist), kwenye Mnet pia nimeandaa na kutangaza kipindi cha Muziki Africa Magic
kinachoruka kupitia Africa Magic Swahili hiyo ilikuwa mwaka 2008,”anasema.

MAFANIKIO

Mwaka 2008 ulikuwa ni mzuri kwake kwani kipindi hicho ndipo alipoanza kupata matunda ya sanaa yake, aliweza kupata dili la kutumbuiza kwenye jumba la Big Brother 3 akiungana na mastaa wengine wa Bongo waliopata mwaliko huo.

“mimi mbali na kufanya filamu ni nafanya sanaa ya mazingaombwe, hii ni sanaaambayo imekuwa ikihusishwa na ushirikina lakini ukweli ni kwamba ni sanaa inayopendwa sana Afrika Kusini na nchi zingine, mazingaombwe ndiyo yalinipa dili la kutumbuiza Big Brother nikiwa na kina Fid Q, Witness, Adam Mchomvu na Zahir Ally Zorro, anasema Forlie.

MAZINGAOMBWE YAMKUTANISHA NA VIONGOZI

Forlie Kacha anasema mbali na kufanya sanaa zingine yeye amefanikiwa baada ya kuwa ‘Magician’ (Mwana maziangombwe), sanaa iliyomkutanisha na viongozi mbalimbali wa serikali hapa nchini, Ulaya na Amerika.

“Nilipotoka Afrika Kusini niliweza kupata nafasi ya kufanya sanaa hii kwenye sherehe kadhaa za serikali, nakumbuka nimewahi kutumbuiza kwenye kampeni ya Malaria Zinduka Project ilikuwa Leaders Club.Pia nimecheza mazingaombwe mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu,Mizengo Pinda Ikulu ndogo ya Dodoma, Miss Nyanda za Juu Kusini na kwenye Miss Reds Tanzania, ” anasema.

Anasema sanaa hiyo ilimpa fedha nyingi akiwa Afrika Kusini kwani aliweza kupata nafasi ya kuonyesha kipaji hicho kwenye kumbi mbalimbali za usiku kwenye majiji ya Johanesburg, Pretoria na Jorburg.

HATOISAHAU HII

Msanii huyu anasema moja ya matukio ambayo hawezi kuja kuyasahau na yalimpa moyo wa kuendelea kupambana ni pale alipopata mwaliko wa kwenye kutumbuiza mbele ya rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na kufanikiwa kukonga nyoyo za wageni waalikwa.

“Binafsi huwa nafurahi ninapoona kazi zangu zinapendwa na watu wakubwa duniani, sikumbuki mwaka nadhani ilikuwa mwaka 2010 au 2011 hivi nilipata nafasi ya kuhudhuria kwenye sherehe za uhuru Afrika Kusini, kupitia Mazingaombwe yangu marais kama Thabo Mbeki, Jacob Zuma, marais wengine wa Afrika na wageni waalikwa waliohudhuria ile sherehe waliondoka na kumbukumbu yangu kwa shoo kali niliyoifanya pale,” anasema Forlie.
Nimecheza Mazingaombwe Ikulu ya Afrika Kusini wakati wa sherehe za Uhuru.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -