Saturday, November 28, 2020

Francis Cheka: Dullah Mbabe anatafuta kiki

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

TANZANIA imejaaliwa kuwa na mabondia wengi wa ngumi za kulipwa wanaochipukia na wa zamani, wakiwamo  wale wanaotoka katika ukoo wa mzee Matumla, yaani Rashind, Mbwana, Hassan na wadogo zao.

Ndani ya miaka 10 kama si 20, kumeibuka mabondia wengi wenye uwezo wa hali ya juu, akiwamo Francis Cheka anayetakwa kuchangia kwa kiasi fulani kumaliza utawala wa familia ya mzee Matumla katika mchezo huo.

Cheka aliyeanza ngumi mwaka 2000 na kuweka rekodi ya kushika nafasi ya 55 katika viwango vya dunia uzito wa ‘supper middle weight’ kati ya 1258, anashika nafasi ya kwanza Tanzania kwa ubora kulingana na viwango vya tovuti ya BoxRec.

Katika umri wake wa miaka 34, ameshacheza mapambano 43 ya ndani na nje ya nchi. Ameshinda 32 kati ya hayo 17 ya ‘knockout’, amepoteza tisa kati ya hayo sita kwa ‘knockout’ na kutoka sare mara mbili.

Hakuna asiyemjua Cheka japo kwa siku za karibuni ameamua kukaa pembeni, wengi wakiamini utawala wake umemalizika.

BINGWA limemtafuta Cheka ili kuzungumza naye masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na pambano lake dhidi ya Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’.

Dullah Mbabe nitapigana naye hata nyumbani kwake

Siku chache baada ya bondia Dullah Mbabe kugoma kupigana na Cheka mkoani Morogoro, mkogwe huyo wa ngumi ameibuka na kusema kuwa anajua mpinzani wake anatafuta kiki.

“Najua Dullah anatafuta ‘kiki’, nini Morogoro, nipo tayari kupigana naye hata nyumbani kwake au nimwandalie pambano Tabora tumalize ubishi?

“Dullah ana pambano gani la maana zaidi ya lile la kumtwanga Mchina sasa akaangalie rekodi zangu, pambano lake watu waliingia kwa 15000, wakati mimi kwa mara ya mwisho watu waliingia kwa 100,000.

Ninachoweza kumwambia aache kelele aitafute sifa kwa jina langu kama anataka pambano kweli nipo tayari kupigana naye popote pale.

Ajikita kwenye upromota

Baada ya kuwa nje ya ulingo kwa muda, Cheka amesema kwa sasa ameamua kuwa promota wa ngumi na tayari amefungua Kampuni ya Cheka Promotion.

“Cheka Promotion inashughulikia uandaaji wa mapambano ambapo kwa kuanzia tumeandaa pambano letu la kwanza Desemba 9 ambalo litakuwa la Cosmas Cheka na bondia kutoka Kenya,” anasema Cheka.

Fedha nyingi aliyowahi kupata katika ngumi

Cheka ambaye ni bingwa wa zamani wa WBC na WBO sanjari na yale ya Afrika ya UBO, IBF, WBO, alisema fedha nyingi alizopata ni Sh milioni 10 ambayo alicheza pambano Russia Desemba 2012 na kupigwa kwa Knock Out (KO) raundi ya nne.

“Pambano lile sikujiandaa na nilipata fedha hiyo naamini ndio fedha ndefu niliyowahi kupata kwenye kazi yangu hii ya ngumi,” alisema.

Mapambano mengine mengi ya nchini nimekuwa nikiambulia Sh milioni tatu mpaka nne baada ya fedha za maandalizi, kumlipa kocha na vifaa.

Pambano nililocheza na Mmarekani la ubingwa wa dunia nilipewa Sh milioni tano za maandalizi, nikaweka kambi Nairobi kila kitu nalipa mwenyewe mpaka kumlipa kocha.

Ampigia saluti marehemu Mashali kwa kumtwanga

Cheka amempa saluti marehemu Mashali ambaye enzi za uhai wake alimchapa katika pambano lao la Morogoro lililokuwa la marudiano.

Cheka na Mashali wamepigana mara mbili ambapo kwenye pambano la awali la raundi ya 12 lililofanyika katika ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam na Cheka kushinda pambano hilo katika raundi ya 10 kwa knock out (KO).

Baada ya pambano hilo, wawili hao walirudiana mkoani Morogoro muda mfupi baada ya Cheka kutoka gerezani, katika pambano hilo la marudiano Mashali alifanikiwa kushinda kwa pointi.

“Siku ile wala sitaki kudanganya, Mashali alinipiga kweli makonde ya maana ndio maana hata majaji walimpa ushindi nampa saluti na namuombea huko aliko,” anasema.

Hajawahi kushinda nje ya nchi

Kwenye rekodi zake Cheka hajawahi kushinda katika mapambano yaliyochezwa nje ya Tanzania.

Mwaka 2005 aliwahi kucheza dhidi ya Robert Stieglitz nchini Ujerumani na kupigwa kwa ‘knockout’ (KO), pia 2007 alicheza Uingereza dhidi ya Paul Smith na 2008 dhidi ya Geard Ajetovic na kupigwa kwa pointi na mwaka huo alicheza na Muingereza mwingine Mathew Maclin na kupigwa tena kwa pointi.

2013 alicheza dhidi ya Mjerumani, Uensal Arik na baadaye mwaka huo kucheza na Mrusi, Fedor Chudinov.

Ila kwa Kwa Tanzania nyota yake imeng’ara kwa kuwachapa mabondia kadhaa kama Rashid na Hassan Matumla, Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’, Karama Nyilawila, Mada Maugo na Japhet Kaseba.

Amlilia Nape kushikiliwa kwa hati yake ya kusafiria

Cheka amemlilia Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, kumkomboa kutoka mikononi mwa mapromota wababaishaji ambao wamezuia hati yake ya kusafiria (passport).

“Toka nimemaliza pambano langu na Mmarekani, promota Juma Ndambile ameshikilia hati yangu ya kusafiria mpaka leo, Waziri wangu, hebu angalia mapromota wanavyotutesa, kwanini ashikilie haki yangu mpaka leo?

“Nimekuwa nikilalamika kila siku lakini mpaka sasa sijapata jibu, ehh Waziri wangu nisaidie kulisimamia hili ili nipate haki yangu.”
Takwimu za Cheka

Jina:        Francis Cheka

Kuzaliwa:     Aprili 15, 1982

Pambano:     ‘Super middle’

Urefu:           5’10.5”/ sm 179

Uzito:           kg 75.7

Nchi:       Tanzania

Shinda 32 (KO 17) + Poteza 9 (KO 5) + sare 2=43.

Zaibabykhalid@yahoo.com.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -