Monday, October 26, 2020

Fundi Mkhitaryan, yupo kama hayupo Manchester

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA ALLY KAMWE,

UNAWEZA kujiuliza swali hili na ukakosa jibu. Jose Mourinho aliwaza nini kuwasajili wachezaji wabunifu kama Paul Pogba na Henrikh Mkhitaryan ikiwa bado ana mipango ya kucheza soka la kujilinda?

Pengine msimu huu Manchester United imekusanya kikosi chenye wachezaji wabunifu zaidi lakini jambo la kushangaza ni vipi Mourinho anaanza pambano dhidi ya Chelsea akiwa na lengo la kupata pointi moja.

Kipindi cha kwanza Jesse Lingard na Marcus Rashford walicheza muda mwingi kwenye mstari wa mabeki wa kati, ni ngumu kuona uwezo kama mfumo utawapa zaidi majukumu ya kujilinda.

Kwanini Mourinho anashindwa kumuamini Mkhitaryan na kuendelea kumtumia Marouane Fellaini? Je, Mkhitaryan ni mgonjwa?

Kama si mgonjwa, tatizo nini? Jose hafurahishwi na uchezaji wake? Mpaka sasa jicho la shabiki wa kawaida kabisa limeshajiridhisha kuwa Fellaini hawezi kuwa ‘patna’ wa Paul Pogba. Kwanini Mourinho ameendelea kubisha?

Bila shaka mpaka sasa uongozi wa Manchester United utakuwa kwenye mtihani wa kuangalia namna ya kumbadili Mourinho kabla hajawabadilisha wao.

Watu wanasema wachezaji wanatakiwa kubadilika na kuingia kwenye mfumo wa kocha, lakini kwa sasa Mourinho ndiye anayetakiwa kubadilisha mbinu zake na kuendana na faslafa na tamaduni za Man United.

Mashabiki wa Manchester United wanataka kuiona timu yao ikishambulia na si kujilinda, hakuna raha kubwa kama kushinda na kucheza soka la kuvutia.

Na kwa aina ya wachezaji wa United, uamuzi upo kwa Mourinho tu kuamua kuwafurahisha mashabiki wake, kwanini hampi nafasi Henrikh Mkhitaryan? Nani ana jibu sahihi la swali hili?

Tangu atue United akitokea Borussia Dortmund, Henrikh ameanza mchezo mmoja tu dhidi ya Manchester City na alitolewa baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Wengi hawaelewi kwanini Jose Mourinho anashindwa kumuamini Mkhitaryan japo rekodi ya kiungo huyu kutoka Armenia zinaonyesha amekuwa akipata shida kila anapoingia kwenye timu mpya.

Alianza soka lake na klabu ya Pyunik Yerevan ya Armenia mwaka 2006, akahamia nchini Ukraine kwenye klabu ya Metalurh Donetsk mwaka 2009, kisha kupata nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa mwaka 2010 alipojiunga na Shakhtar Donetsk.

Miaka mitatu baadaye alijiunga na wabishi wa Ujerumani, Borussia Dortmund alipocheza kwa mafanikio makubwa.

Mircea Lucescu aliyewahi kuwa kocha Mkhitaryan wakati akiwa Shakhtar, aliwahi kueleza namna alivyopata shida na Henrik msimu wa kwanza alipomsajili.

Na tiba pekee aliyoigundua kwa Mkhitaryan ni kumpanga nyuma ya mshambuliaji alipofunga mabao 25 kwenye michezo 29 ya ligi, hali iliyowapelekea Dortmund kutoa kiasi cha pauni mil 20 kumsajili.

Benchi la ufundi la Borussia litakwambia stori ileile kuhusu Mkhitaryan, hakuna msimu mzuri alipowasili hadi mwaka wa tatu alipofunga mabao 23 kwenye mechi 51 na kutimkia Manchester United.

“Henrikh amekaa Dortmund kwa miaka mitatu,” alikaririwa kiungo wa zamani wa Dortmund, Ilkay Gundogan. “Alifanya vyema msimu wake wa mwisho tu, misimu miwili ya mwanzo alipata shida sana.”

Bosi wa Dortmund, Hans-Joachim Watzke alirudia kusema jambo hilo hilo wiki chache zilizopita akimuelezea Mkhitaryan.

“Unapocheza kwenye timu iliyotengenezwa nyuma yako kama tulivyofanya Dortmund, lazima mambo yawe rahisi kwa mchezaji yeyote yule duniani. Nafikiri Mkhitaryan alifanya haraka kuondoka hapa.”

Ni kweli na hakuna wa kuweza kupinga hili, Mkhitaryan amekuwa na rekodi mbaya kila anapojiunga na timu mpya lakini hili halifichi ubora wake.

Mourinho anatakiwa akumbuke alichohitaji wakati alipokuwa tayari kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili Mkhitaryan, alimsajili ili akae benchi?

Wachezaji aina ya Mkhitaryan wanapenda kucheza mechi kubwa, wanapenda kuonekana wakifanya makubwa huko, bila shaka hili la kuwekwa benchi litakuwa likimpa hisia tofauti.

Ana miaka 27, ni kipindi kizuri kwake kucheza soka la kikubwa na kutengeneza historia yake. Kuna kitu kimejificha miguuni mwake, ni kazi ya Mourinho kukifichua, ampe nafasi fundi huyu!

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -