Sunday, October 25, 2020

FUNGA MWAKA… NI VITA YA KUFUNGA MWAKA EPL

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

LONDON, England

NI vita ya funga mwaka Ligi Kuu England, hivi ndivyo pengine unavyoweza kusema wakati ukizungumzia mechi za leo katika michuano hiyo.

Msemo huo unatokana na kwamba, miamba mitatu inayofukuzana katika mbio za kutwaa taji hilo itashuka tena kwenye viwanja tofauti, huku ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi zao zilizopita.

 *Chelsea vs Stoke City

Katika michezo iliyopita vinara  wanaoongoza ligi hiyo, Chelsea, waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bournemouth, wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Stamford Bridge na leo tena watakuwa kwenye dimba hilo wakiumana na Stoke City.

Endapo watashinda, basi watakuwa wamezidi kujichimbia keleleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 49 na hivyo kuzidi kuwaacha mbali wapinzani wao wanaofukuzana nao katika mbio za ubingwa.

Hadi sasa Chelsea wameshajikusanyia pointi 46 katika  michezo 18, huku Stoke City wao wakiwa na pointi 21 walizozikusanya katika michezo kama hiyo.

Rekodi zinaonesha kuwa, Chelsea ndio wamekuwa wakiibuka na ushindi mara nyingi, kwani katika mechi 18 imeshinda 15 ikipoteza mbili na huku miamba hao wakitoshana nguvu  mara 11.

*Man United     v   Middlesbrough

Mbali na mtanange huo, uhondo mwingine utakuwa kwenye Uwanja Old Trafford ambapo mashetani wekundu wao watakuwa wakipamba na Middlesbrough   ili kuona kama watajikwamua katika nafasi yao ya sita ambayo imewaandama kwa muda mrefu.

Kama walivyo The Blues, katika mchezo uliopita Man Utd nao waliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland na hivyo kufanikiwa kufikisha pointi 33 na endapo watashinda watakuwa wameifikia Tottenham, ambayo inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi  36 na huku ikiwa imebakiza pointi moja kuifikia Arsenal ambayo ipo nafasi ya nne.

Kwa sasa vijana  hao wa Kocha Jose Mourinho  wanaonekana kuanza kurejea kwenye ubora wao baada ya kushinda mechi nne mfululizo, ukiwamo ushindi huo wa  3-1 dhidi ya Sunderland.

Mbali na hilo, pia uhondo mwingine utakuwa ni kwa straika wao, Zlatan Ibrahimovic, ambaye anaonekana kuwa na uchu wa kuzifumania nyavu, kwani raia huyo wa Sweden ameshafunga mabao  10  katika michuano hiyo ya Ligi Kuu  pekee na huku matano akiwa ameyafunga katika mechi tano zilizopita.

Wakati Man Utd  watakuwa wakitaka kutochafuliwa rekodi yao hiyo, kwa upande wao Middlesbrough nao watakuwa wakitaka kuzinduka baada ya kuchapwa katika mchezo wao wa mwisho kwa bao  1-0  dhidi ya  Burnley na hivyo kuwaacha wakiwa hawana ushindi katika  michezo 8  waliyocheza wakiwa ugenini tangu waliposhinda  2-1 dhidi ya  Sunderland  siku ya pili tangu ligi ianze.

Kibaya zaidi timu hiyo imepoteza michezo mitatu kati ya minne iliyopita na kuna hali ya hatari ya kunyemelewa na janga  kwa  Teessiders kushuka daraja.

Kwa sasa Middlesbrough inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi na inatenganishwa na tofauti ya pointi nne kutoka ukanda wa kushuka daraja.

Middlesbrough iliitembelea Manchester United  msimu uliopita katika michuano ya Kombe la Ligi, wakati huo likiitwa Capital One  na kuondoka na ushindi wa mikwaju ya penalti, lakini Man Utd haijawahi kufungwa katika michezo 10 waliyokutana na  Middlesbrough ambapo imeshinda sita na kutoka sare minne.

*Liverpool vs Manchester City

Pia uhondo mwingine wa kufunga mwaka utakuwa katika Uwanja wa Anfield ambako Liverpool  watakuwa wakiikaribisha Manchester City.

Kama wenzake, Liverpool  mwanzoni mwa wiki hii iliondoka na ushindi mnono wa mabao  4-1  ikiwa nyumbani dhidi ya  Stoke City na hivyo kuongeza rekodi ya kutofungwa ikiwa Anfield  michezo 10 katika mashindano yote, ikiwamo nane ya Ligi Kuu.

Kiwango kinachooneshwa na Reds kwa sasa ikiwa nyumbani kinaonekana msimu huu kuwa kizuri zaidi ambapo ikiwa katika uwanja huo imeweza kukusanya pointi 20 kati ya 24.

Vijana hao wa Jurgen Klopp wataingia katika mchezo huo wakiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi 40, ikiwa ni pointi moja zaidi dhidi ya wapinzani wao.

Kwa upande wao, Manchester City wameonekana kuzinduka baada ya kupoteza mechi mbili na sasa wameshinda tatu mfululizo na wamefunga mabao saba na kuruhusu  moja katika michezo mitatu ya ligi.

Jambo jingine, Manchester City wanashika nafasi ya pili kwa kufanya vizuri msimu huu wakiwa ugenini ambapo wameweza kukusanya pointi 21 katika mechi tisa walizocheza.

Msimu uliopita Liverpool  na  Manchester City zilikutana mara tatu na Reds ndio walionekana kuwa wababe baada ya kushinda mara mbili,  ukiwamo wa mabao  4-1  wakiwa ugenini na 3-0 wakiwa  Anfield.

Kwa upande wao Man City, walishinda mechi ya tatu katika michuano ya Kombe la Ligi kwa jumla ya mabao  2-1.

Mbali na ushindi huo, Liverpool  imeshinda mechi nne kati ya 10 ilizokutana na Man City, wakati wapinzani wao hao wakishinda mara mbili na huku wakishindwa kuondoka na ushindi katika michezo 13 waliyocheza  Anfield.

Mechi nyingine zitakuwa  ni kati ya

Burnley    dhidi ya   Sunderland,

Swansea City dhidi ya AFC Bournemouth, Southampton dhidi ya West Bromwich  na  Leicester City    itakayokuwa ikiikaribisha West Ham.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -