Tuesday, October 27, 2020

Furaha yako haiwezi kulinganishwa na mwonekano wake

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

KUNA watu wapo katika mahusiano ya kimapenzi lakini ni kama wako utumwani. Hawana amani wala raha, thamani ya mahusiano yao inalindwa na unyonge wao pamoja na uzito wa mifuko yao. Kwao mapenzi si raha wala amani, mahusiano kwao ni kama kuongeza matatizo na matumizi ya kuwafilisi katika maisha yao. Wewe upo katika mahusiano ya namna gani?

Au wewe upo katika mapenzi na mtu anayekufanya mtumwa wa ngono. Hakutafuti wala hakujali mpaka ajisikie hamu ya ngono, unakuwa mzuri pale tu anapotaka penzi lako na si vinginevyo. Mapenzi maana yake amani na furaha. Muonekano wake na kazi yake havina maana kwako kama hupati raha na thamani halisi ya penzi. Ni ujinga kujisifu kuwa na mpenzi tajiri ila anakuuliza na kunyanyasa. Haina maana kuwa na mtu mwenye muonekano wa kusisimua kila mtu ila anakufanya mtumwa katika maisha yako. Amani katika mahusiano yako inatokana na kuwa na mtu makini mwenye kujua thamani na ubora wako katika maisha yake kinyume cha hii ni kinyume cha furaha yako.

Kama upo katika uhusiano na mtu ambaye anakufanya ulie na ujutie kuwa naye, suluhisho si kulia. Tiba si kusema una mikosi. Huna mikosi wala huna bahati mbaya. Kama unajitoa kwa ajili yake kisha hathamini. Kama unaumwa akiumwa ila ukiumwa wewe hajali, anakuulizia hali yako mpaka uanze kujisemesha kwake mtu wa aina hii wa kazi gani?

Furaha ya maisha yako ina thamani kuliko mali na muonekano wako. Hakuna faida ya kuishi kama huna amani na raha. Sasa ya nini kuwa na mtu ambaye anakufanya hata usistahili kuishi? Ni vizuri sana kupigania uhusiano wako, ila ni uzezeta kupigania uhusiano kwa mtu ambaye anaonesha dhahiri hakujali, hakuthamini na zaidi anafanya matendo ya kukudhalilisha.

Huenda ni mzuri sana, huenda utajiri wake unakupa sifa sana mtaani, ila kuna thamani kati ya hivyo kinacholingana na thamani ya maisha yako? Kitaalamu ni kuwa huwezi kufanya vizuri katika maisha kama kila siku wewe ni mtu wa huzuni na fadhaa. Sasa ya nini kumpa mtu thamani katika maisha yake kisha yeye anakuwa kikwazo cha ustawi wako katika maisha?

Ni vema ikafahamika kuwa uamuzi ndiyo kitu kinachoamua hali ya maisha yako katika lolote. Kama ilivyo kuwa ukiamua kufanya kazi kwa bidii na kuwa na matumizi sahihi ya kipato chako ndivyo utakavyojiweka katika nafasi kubwa ya kufanikiwa, ndivyo ilivyo katika uhusiano. Kama ukiamua kujifanya sugu kuvumilia matusi, dharau na usaliti wa mtu wako unaokufanya kila siku uwe mtu wa huzuni badala ya furaha ndivyo kila siku utakavyokuwa unajiweka mbali na furaha halisi katika maisha yako.

Baada ya kujitolea kwa kila kitu kwa mtu wako na yeye kutothamini lolote ni muda sasa wa kuangalia thamani yako katika maisha. Kuna faida kubwa ya kujitenga na mahali panapokupa huzuni bila kujali muonekano wala utajiri uliopo. Unapojitenga na huzuni fahamu ndivyo unavyosogelea furaha. Bila kuachana na huyo anayekuliza na kukufanya mtumwa badala ya mpenzi wake wa thamani, ndivyo unavyojiweka katika nafasi ya kuwa na mtu atakayekuthamini na kujali hali yako. Kuna kanuni moja tu ya kupata unachohitaji katika maisha yako, nayo ni kuachana na usiyoyahitaji. Unataka amani na raha kama ilivyo kwa kila binadamu kamili? Mpe mkono wa kwa heri huyo akuumizae na kukufanya mjinga badala ya thamani bora katika maisha yake.

Kama ilivyo kuwa bila kuacha kazi mbaya huwezi kupata nzuri, ndivyo ilivyo bila kuachana na huyo mwanamke anayezuzuliwa na mapambo ya dunia huwezi kumpata mwanamke mwenye kujua thamani yako na kukufanya ujihisi bora katika maisha yako.

Ugonjwa unaosumbua wengi katika mahusiano yao ni kutojua ukweli katika maisha. Ukweli wa maisha ni kuwa kuachana na kisicho kufaa ni njia ya kupata bora zaidi na kinachokufaa. Hii haiaminiki kwa haraka kwa sababu akili ya binadamu huwa ni ngumu kuamini bila kuona.

Hii dunia ni kubwa na inakupa kila unachohitaji. Bila mwanamuziki Diamond kuacahana na yule Miss Kishawahili Jackline asingeweza kuwa na kina Wema na bila kuachana na Wema asingeweza kuwa na mwanadada makini Zarina Hassan ‘Zari’ ambaye amefanikisha ndoto ya Diamond kuitwa baba.

Maneno haya yakufunze kuwa katika maisha uamuzi wako wa kutoka mahali usipostahili ndiyo hatua ya kufika mahali unapostahili. Ni hivi, kama mtu anakuliza ila unamng’ang’ania kwa sababu yoyote hasa ya kimuonekano, mali au mazoea, basi fahamu huzuni ya maisha yako haitengenezwi na yeye kwa matendo yake bali inaumbwa na wewe kwa uamuzi wako. Furaha ya maisha yako kimahusiano inaamuliwa na uamuzi wako, ukiamua kuwa naye kisa tu unajilaghai kuwa huwezi kupata mwingine kama yeye kimuonekano au kwa ujuzi wake basi jua matokeo ya uongo huo unaolisha akili yako ni wewe kuwa katika huzuni katika kipindi chote cha mahusiano yako. Katika nchi kama Tanzania yenye watu zaidi ya milioni 45 ni utoto kuamini kuwa hakuna mwingine mwenye kujua mapenzi na mwenye muonekano kama yeye ama bora zaidi yake.

 ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -