LONDON, England
MJOMBA wa bondia Tyson Furry, Peter, ambaye pia ni kocha wake, amesema kuwa Anthony Joshua ‘AJ’, anapaswa kujiandaa ipasavyo kwani pambano lake lijalo dhidi ya Wladmir Klitschko April 29, mwaka huu kwenye dimba la Wembley, litakuwa ni jaribio lake kubwa la kwanza tangu kuanza kwake kupambana ulingoni.
Klitschko hakupanda ulingoni tangu alipopoteza mikanda mitatu ya WBO, WBA ‘super’ na IBF kwa Tyson Fury jijini Dusseldorf, Ujerumani Novemba, 2015, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Klitschko kuchapwa katika kipindi cha miaka 11 ya kuzichapa ulingoni.
Furry alidai kuwa, Klitscho ataingia ulingoni akiwa na kumbukumbu ya kichapo kikali alichokipata kutoka kwa mpwa wake, hivyo atajitahidi kumpa changamoto AJ.
“Kwa maoni yangu, Klitschko ana nafasi ya kushinda kwani ni mzoefu lakini itategemea na jinsi gani atakavyoingia mchezoni kwani tangu alipochapwa na Furry, hajaingia ulingoni tena,” aliosema.