Tuesday, January 19, 2021

GERVAS CHILIPWELI: JUDO KWANGU NI KILEVI TOSHA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

 

NA SHARIFA MMASI

JUDO ni miongoni mwa michezo inayochezwa nchini Tanzania na inajitahidi kujikusanyia mashabiki sehemu zote mbili za Muungano, yaani Tanzania Bara na Zanzibar.

Mashabiki hao wanazidi kuongezeka siku hadi siku kutokana na hamasa wanayoipata kupitia kwa wachezaji wa mchezo huo, pale wanapoonyesha ushindani katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.

Gervas Chilipweli (34), licha ya kujikita kwenye mchezo wa judo, yeye ni askari Magereza na ni mchezaji wa timu ya Magereza. Alianza kushiriki mchezo huo mwaka 2010 na hadi sasa anapigania uzito wa kilogramu 81.

BINGWA lilifanya mahojiano na mchezaji huyo, kwa lengo la kujua mambo mengi yanayomhusu ambayo kwa namna moja au nyingine yalikuwa hayafahamiki na wadau mbalimbali wa michezo nchini.

Bingwa: Tangu uanze kucheza judo, umepata faida gani kubwa ambayo kila ukikaa huishi kuifikiria?

Gervas: Moja ya faida kubwa ambayo najivunia nayo kupitia huu mchezo, ni afya yangu, sikufichi huwa sipati homa za mara kwa mara na maradhi madogo madogo kama watu wengine ambao hawachezi mchezo wowote.

Bingwa: Ratiba yako ya mazoezi ikoje kwa siku?

Gervas: Kama kuna michuano yoyote ratiba yangu inafuata maelekezo ya kocha na kama hakuna huwa ninafanya mazoezi kwa siku mara mbili asubuhi na jioni nikiwa nyumbani kwangu.

Bingwa: Kwanini uliamua kucheza judo na si soka au michezo mingine?

Gervas: Dah, kiukweli huu mchezo ninaupenda kutoka moyoni tangu nikiwa mdogo, michezo mingine kama soka, riadha niliwahi kujaribu lakini Mungu alinipangia huku ndio maana napambana nako mpaka kieleweke.

Bingwa: Miaka mingapi imebaki ustaafu kucheza judo?

Gervas: Ha ha ha, yaani hilo futa kabisa katika kichwa chako, sijafikiria kustaafu huu mchezo na nikifanya hivyo nahisi nitakufa kwani tayari umeshaingia kwenye damu.

Bingwa: Kati ya michezo yote unayoifahamu, upi kwako ni mgumu?

Gervas:  Watu wengi wanasema judo ni mchezo wa hatari sana, lakini mimi nafikiri hakuna kitu kigumu kila mchezo una faida na madhara yake endapo utacheza bila kufuata kanuni na taratibu zake.

Bingwa: Kazi gani nyingine inayokuingizia kipato ukiacha uaskari na judo?

Gervas: Kwa kweli nategemea sana kazi yangu ya uaskari Magereza kwani hiyo ndiyo imenifanya leo hii najulikana kupitia judo na ndiyo ninaitegemea katika kuendesha maisha yangu ya kila siku.

Bingwa: Ukiwa kama mdau mkubwa wa michezo, kitu gani umepanga kufanya kwa maendeleo ya michezo nchini?

Gervas:  Kwanza kabisa nina mpango wa kufungua klabu yangu hapo baadaye itakayosaidia kuinua vipaji vya vijana wenye mapenzi na mchezo huu.

Bingwa: Kipaumbele chako kwa vijana watakaojitokeza kitakuwa kwa wanaume au wanawake?

Gervas: Ha ha ha, sitarajii kuweka makundi ya aina hiyo, nitatoa ushirikiano kwa vijana wote watakaojitokeza bila kujali dini, kabila, rangi wala sura ya mtu.

Bingwa: Mahusiano kati ya wachezaji na viongozi wa mchezo huu yako vipi?

Gervas: Wachezaji wote tuna mahusiano mazuri na viongozi wetu wa klabu na hata chama kwa ujumla.

Bingwa: Upi wito wako kwa vijana na Serikali kwa ujumla?

Gervas: Naiomba Serikali izidishe ukaribu na wachezaji wa mchezo huu, kwa kutatua matatizo yanayotafuna maendeleo ya judo nchini, naamini hakuna kinachoshindikana, tunawaamini viongozi wetu waliopo madarakani, hivyo nawaomba wasitusahau.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -