Friday, October 23, 2020

Giggs adai Mourinho kamvuruga Rooney

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

MANCHESTER, England

MKONGWE wa Manchester United, Ryan Giggs, amesema Wayne Rooney amevurugwa na kocha wake Jose Mourinho.

Nyota huyo wa Wales anaamini kwamba kumchezesha Rooney kwenye nafasi ya zamani ya ushambuliaji kumemwathiri sana msimu huu.

Rooney aliwekwa benchi na Mourinho baada ya kuanza msimu vibaya na pia aliwekwa benchi na kocha muda wa England, Gareth Southgate, katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 dhidi ya Slovenia, mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 0-0.

Lakini mkongwe wa United Giggs, ambaye amenyakua mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na nahodha huyo wa England, amesema Rooney anaweza kujituma mwenyewe kuweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo na timu ya taifa.

Baada ya mchezaji huyo alianza kucheza soka kama winga, lakini katika miaka ya hivi karibuni, Giggs alikuwa aking’ara sana katika nafasi ya kiungo.

Alicheza mechi chache kutokana na kuwa na umri mkubwa, lakini alitoa mchango mkubwa ambao walinyakua taji la ligi kabla hajastaafu akiwa na rekodi ya kubeba mataji 13 ya Ligi Kuu England.

Giggs anaamini Rooney, ambaye amecheza soka katika kiwango cha juu tangu akiwa na umri wa miaka 16, anaelekea kwenye mabadiliko kama yaliyomkumba yeye.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 42, aliiambia televisheni ya ITV: “Namuona Rooney akiwa katika kipindi cha mpito, hata mimi nilipokuwa na umri wa miaka 29 au 30, nikiwa winga na nilipoanza kushindwa kuwapenya mabeki nilihamia kwenye nafasi nyingine.”

“Namsikitikia sana Rooney, msimu uliopita kwenye klabu yake na timu ya taifa ya England alicheza kama kiungo, majira ya kiangazi akaambiwa na Mourinho atacheza kama namba tisa au 10, inaonekana hilo limemchanganya.”

Rooney alizomewa kwenye Uwanja wa Wembley kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Malta, lakini Giggs haamini kwamba huo ndio mwisho wa kiwango kizuri cha Rooney kwenye soka lake.

“Njia pekee ambayo Rooney anaweza kujirudisha kwenye kiwango chake ni mazoezini,” aliongeza Giggs.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -