Tuesday, October 20, 2020

Kwa heri Wawa soka la bongo ‘litakumiss’

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NI mara chache kwenye soka la bongo mchezaji wa kimataifa ametokea na kukubalika kwenye macho ya wadau na mashabiki wote wa soka nchini.

Licha ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kuvutia wachezaji wengi wa kigeni, lakini wale ambao wamefanikiwa kubaki kwenye akili za wengi ni wachache sana (hii inatokana na 10% zinazopigwa mara kwa mara kwenye usajili).

Na uchache huu ndio siku zote huumiza sana moyo wangu, pale ninaposhuhudia fundi wa kigeni akiondoka kwenye klabu kwa sababu najua kuwa kuondoka kwake kunaweza kukawa ni tiketi ya kuletwa watu kama akina Jama Mba au Kanu Mbiyavanga.

Maana najua nafasi zenyewe za wachezaji wa kigeni chache, wakati wapigaji nao wanazitolea macho hizo hizo kwa ajili ya kutengeneza uwezekano wa kula asilimia 10, hivyo kama mdau wa soka nimesikitishwa sana na kuondoka kwa Serge Pascal Wawa kutoka pale Azam.

Nani alikuwa hajui uwezo wa huyu mtu ambaye wadau wa soka walimtungia jina la Waziri wa Ulinzi, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza kama beki wa kati, huku akiwa kiongozi wa wenzake.

Lakini, Azam wamemuacha arudi El Merreikh, binafsi naamini pengo aliloliacha Chamazi ni kubwa kuliko wenyewe wanavyodhani na hilo lilishaonekana tangu mzunguko wa kwanza wa msimu huu.

Wakati akiwa majeruhi na kukosa mechi zote 15 za mzunguko wa kwanza, Azam imeruhusu mabao 14 na kufungwa michezo minne, idadi ambayo ni kubwa kulinganisha na msimu uliopita, walipokuwa wakichuana na Yanga kwenye mbio za ubingwa.

Bila Wawa kwenye ukuta wa Azam, timu hiyo imeonekana ya kawaida, japokuwa akina Aggrey Morris wanapambana kuziba pengo lake, lakini bado hawajafanikiwa katika hilo.

Inawezekana umri wa Wawa umekwenda, lakini binafsi naamini bado alikuwa na nafasi kubwa kwenye kikosi cha Azam na huu uamuzi wa kushindwa kumfunga na mkataba mpya utawatesa sana msimu huu.

Licha ya kusajili kwa Mghana Daniel Amour, lakini ukuta wa Azam bado ulikuwa unamhitaji Wawa, kwa sababu hata kwenye mechi 15 walizokuwa na ukuta mbovu, staa huyo mpya kutoka Medeama alikuwepo kikosini.

Binafsi nilitarajia baada ya Wawa kuondoka rasmi Azam ingeziba pengo lake kwa kuleta beki wa kati wa kiwango chake pale Chamazi, lakini cha ajabu ni kuwa, timu hiyo ndiyo kwanza imeongeza mastraika.

Ujio wa Enock Atta kutoka Medeama na usajili mpya wa  Yahaya Mohammed na Samuel Afful wote kutoka Ghana umeniacha nikiwaza iwapo Azam wanafahamu kama wana tatizo nyuma, wakati huu wakiimarisha safu ya ushambuliaji.

Siku zote muda ndiyo utatoa hukumu sahihi kwa hiki kilichofanywa Chamazi, lakini kwa sasa mimi binafsi acha nimtakie kila la kheri Wawa, mchezaji ambaye akiwa uwanjani bila kujali timu yako unaweza kujikuta ukimpigia makofi kutokana na utulivu wake.

Najua nitakosa tena vitu vyake uwanjani, lakini hakuna jinsi, maana viongozi wa Azam ndio walikuwa wana sauti ya mwisho, lakini wameshindwa kumbakisha, hivyo mimi sina budi kusikitika kimya kimya tu kwa sababu wenyewe wameshaamua.

Naamini mashabiki wa Chamazi wataendelea kuimba jina lake, kama ambavyo wale wa Simba wanajuta kumuacha Amiss Tambwe au wale wa Yanga ambao hadi leo hii wametofautiana kwenye jibu la swali la je, Andrey Coutinho arudi au asirudi?

Wakati mwingine soka linatufundisha kukubali kumuachia mchezaji kama ambavyo Manchester United iliwahi kukubali kumuachia Cristiano Ronaldo, lakini hii si sababu ya mimi kuacha kusikitika kila nikifikiria kuwa fundi wa mpira mmoja kapotea kwenye viwanja vyetu vya VPL.

Mengi aliyokuwa akiyafanya Wawa uwanjani ni nadra sana kukutana nayo miongoni mwa wachezaji wa VPL, hasa mabeki, ndiyo maana nasikitika kuona ameondoka tena bure! Aibu hii!

Kwa ubora wa Wawa, angalau Azam wangepata hata dau kidogo, lakini ule uzembe wetu wa kusubiri mkataba uishe ndiyo watu wakae mezani na mchezaji umeendelea kuumiza timu zetu.

Nitaumia zaidi kama hawa waliokuja Azam kuziba nafasi ya Wawa ili kutimiza wachezaji saba wa kigeni watashindwa kuonyesha kiwango kama ambavyo Pape Nd’aw alishindwa kuziba pengo la Tambwe Msimbazi.

Sema potelea mbali, wenyewe ndiyo wameamua, mimi sina jinsi zaidi ya kumtakia Wawa kila la heri, maana naamini yeye ni mmoja kati ya wachezaji wachache ambao wamewahi kulitendea haki jina la wachezaji wa kimataifa kwenye soka la bongo.

Natumaini utafanikiwa huko Sudan alikoenda kuendelea kutafuta maisha, ila hata ukiwa huko, amini kuwa tutakukumbuka na pindi wakikufuata urudi nchini usisite kubeba vyako na kutua tena Dar es Salaam kama ambavyo Emmanuel Okwi amekuwa akifanya, kwa sababu naamini Bongo kuna wengi wanakukubali.

Maana binafsi naamini kwa mashabiki wa kweli wa soka ni ngumu kumkataa Wawa, kutokana na ubora wake na akili yake akiwa kama beki wa kati, kila la heri kijana, tunatumaini siku moja utarudi tena Tanzania kuendelea ulipoishia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -