Sunday, January 17, 2021

GRIEZMANN AWAGWAYA MESSI, RONALDO TUZO YA  BALLON D´OR  

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MADRID, Hispania


STRAIKA wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, anaonekana kuwagwaya nyota wenzake, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, katika mbio za kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia,  Ballon d’Or, baada ya kusema kuwa ana nafasi ndogo kubeba  taji hilo kama vinara hao bado wapo kwenye gemu.

Staa huyo wa  Barcelona na mwenzake wa  Real Madrid  wameshatwaa tuzo hiyo mara nane ambapo Messi ameshaibeba mara tano na Ronaldo  mara tatu.

Mwaka huu Griezmann anatarajia kuletea ushindani dhidi ya vinara hao, baada ya kuisaidia Atletico kufika fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na kuing’arisha Ufaransa wakati wa fainali za Mataifa ya Ulaya, Euro 2016, ambapo walifungwa na Ureno katika mchezo huo.

Hata hivyo, pamoja na hali hiyo, staa huyo anawagwaya vinara hao kutokana na mafanikio waliyonayo katika ngazi ya klabu na ya timu zao za taifa.

“Tuzo ya   Ballon d’Or ni moja kati ya malengo yangu, lakini itachukua muda kama  Ronaldo  na Messi  watakuwa bado wapo kwenye gemu,” Griezmann aliuambia mtandao wa  Telefoot.

“Cristiano Ronaldo anaweza kuendelea kucheza kwa muda wa miaka hadi 10 ijayo, hivyo ni jukumu langu kuendelea kujituma ili niweze kufikia ngazi hiyo na nimekuwa nikifanya hivyo kila siku ili niweze kufanya vizuri,” aliongeza staa huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -