Sunday, November 29, 2020

Guardiola akaribishwa England, Man United yabanwa nyumbani

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

Tottenham imemuonyesha kwa mara ya kwanza Pep Guardiola uchungu wa kufungwa tangu atue Ligi Kuu England, baada ya kuichapa Manchester City mabao 2-0, huku mahasimu wao, Manchester United, wakitoka sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford, dhidi ya Stoke City.

Spurs walianza kwa kasi mchezo huo uliochezwa White Hart Lane na kupata bao dakika ya tisa, baada ya beki wa Man City, Aleksandar Kolarov kujifunga, kabla ya Dele Alli kufunga bao la pili dakika saba kabla ya mapumziko.

City, ambao wamefungwa kwa mara ya kwanza wakiwa chini ya Guardiola, walishindwa kucheza katika kiwango chao ambacho kiliwasaidia kushinda mechi sita za msimu huu wa Ligi Kuu England.

Pia bahati ilikuwa nzuri kwa Man City, baada ya Erik Lamela kukosa penalti iliyookolewa na mlinda mlango, Claudio Bravo.

Pamoja na Man City kupambana ili kuweza kubadilisha matokeo, lakini Spurs walikuwa makini na kuendelea na kiwango chao kizuri ambacho kwa mara ya mwisho kuwa kwenye makali kama haya ilikuwa msimu wa 1960/61.

Kwa ushindi huo, kikosi hicho kinachonolewa na Mauricio Pochettino,  kimepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi moja nyuma ya City, wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 18.

Mahasimu wa Man City, Manchester United, walitoka sare hiyo ya 1-1, kufuatia Joe Allen kuisawazishia Stoke City, baada ya Anthony Martial kuifungia klabu hiyo ya Old Trafford bao la kuongoza.

United walishindwa kutumia nafasi zao za wazi katika kipindi cha kwanza hadi alipoingia Martial na kufunga bao dakika ya 69.

Lakini mpango wao wa kulinda bao lao huku zikiwa zimebaki dakika nane, kulimsaidia Allen kutumia krosi ya Jonathan Walters, ambayo iligonga mwamba na kufunga bao hilo na kukiacha kikosi cha Jose Mourinho kushinda mechi moja kati ya nne walizocheza.

Vikosi hivyo havikufanya mabadiliko makubwa, ambapo Wayne Rooney, ambaye alionyesha kiwango kizuri kwenye Ligi ya Europa akitokea benchi, bado hakupewa kuanza kwenye kikosi cha kwanza katika mechi ya tatu mfululizo.

Mshambuliaji wa Man United, Zlatan Ibrahimovic, aliyesaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zorya kwenye Ligi ya Europa, alikosa bao dakika ya saba ya mchezo huo akiwa ndani ya eneno la hatari, baada ya mlinda mlango wa Stoke City, Lee Grant, ambaye alicheza vizuri kuokoa shuti la nyota huyo wa Sweden.

Pogba alipoteza nafasi mbili za wazi, ambapo ya kwanza alikuwa ndani ya eneo la hatari, kabla ya kichwa chake kugonga mwamba na mpira kurejea uwanjani.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -