Saturday, November 28, 2020

GUARDIOLA ANA NGUVU SANA AISEE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

IKIWA si zaidi ya miezi tisa tangu alipopewa kibarua cha kuinoa Manchester City, kocha Pep Guardiola, anatajwa kuwa ndiye kocha mwenye nguvu kubwa Ligi Kuu Engand.

Inaelezwa kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich, anapoondoka lazima timu aliyokuwa akiinoa iyumbe kwa muda fulani.

Alipochomoka Man City, aliondoka na aliyekuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Ferran Soriano, kisha kumchukua mkurugenzi wa soka, Txiki Begiristain.

 

Licha ya kikosi chake kutokuwa na mwenendo wa kuridhisha kivile, tayari mabosi wake pale Etihad wakiongozwa na mmiliki Sheikh Mansour na Mwenyekiti Khaldoon Al Mubarak, wameshasema wanamwamini na wanamuunga mkono katika kila hatua.

Hata hivyo, taarifa za nje ni kwamba mwezi uliopita uongozi wa Man City uliweka wazi kuwa utakabidhi mamlaka yote ya usajili kwa Guardiola.

Hiyo ni kwamba kocha huyo raia wa Hispania ndiye atakayekuwa na sauti ya mwisho kwenye sera ya usajili na mikataba mipya kwa wachezaji wa klabu hiyo.

Lakini pia, kocha huyo alikiri kuwa sasa ana mamlaka makubwa kuliko katika klabu zote alizowahi kufundisha.

Man City chini ya bilionea Sheikh Mansour aliyeinunua klabu hiyo mwaka 2008, wameonekana kumwamini Guardiola kuliko hata ilivyokuwa kwa watangulizi wake Mark Hughes, Roberto Mancini na Manuel Pellegrini.

Lakini pia, Guardiola amekuwa na mawasiliano mazuri na wasaidizi wake Mikel Arteta, Domenec Torrent na Roldolfo Borrell.

Mbali na hao, uhusiano wake mzuri na Carles Planchart ambaye ni mchambuzi wa video na Lorenzo ­Buenaventura anayehusika na masuala ya ‘fitness’ ya wachezaji, umekuwa chachu ya kukubalika zaidi Etihad.

Nguvu kubwa aliyonayo Guardiola klabuni hapo inachagizwa pia na kitendo chake cha kuendelea kuwaamini na kuendelea kuwatumia wafanyakazi aliowakuta Etihad.

Mfano; bado amekuwa akinufaika na huduma ya Brian Marwood ambaye tangu zamani alikuwa mtawala wa soka klabuni hapo.

Tamko hilo la uongozi linakuja huku ikidaiwa kuwa kumekuwa na watu ndani ya Man City wanaompinga Guardiola katika harakati zake za kuifanya Man City kuwa na mwonekano wa Barca.

Chanzo kimoja cha habari kutoka klabuni hapo kiliuambia mtandao wa Mirror: “Muda mwingi, nguvu na fedha zimetumika katika mipango ya Pep ambayo haina ‘Plan B’ ikiwa itashindikana.

“Ferran (Sorino) na Txiki (Begiristain) wameanza kuchoshwa na majanga ya Pep (Giardola) na hiyo ni hatari ikiwa mmoja wao ataondoka. Kama mmoja ataondoka, mwingine atafuata.

“Hebu fikiria kilichotokea Man United wakati Sir Alex Ferguson na David Gill walipoondoka.”

Asilimia 10 ya pauni milioni 200 zilizomwagwa na uongozi wa Man City kujenga kambi ya kisasa karibu na Uwanja wa Etihad, ilitumika kununua kifaa maalumu cha kutibu wachezaji majeruhi.

Hata hivyo, bado Guardiola alikuwa akisisitiza wachezaji wake, wakiwamo Vincent Kompany, Kevin De Bruyne na Gabriel Jesus, kupelekwa kwa daktari anayeishi mjini Barcelona, Dk. Ramon Cugat kwa matibabu.

Kwa sasa Man City wamemchukua Dk. Eduardo Mauri ambaye amependekezwa na Dk Cugat. Mtaalamu huyo wa afya amekuwa akifanya kazi akishirikiana na Silvia Tremoleda.

Ingawa uongozi unampa madaraka yote, wapo ambao wanahoji juu ya anachokifanya Guardiola katika kutimiza ndoto za Man City. “Inaonekana kama anataka kuileta Barcelona hapa Manchester kuliko kuijenga Manchester City,” kilisema chanzo hicho.

“Watu wa hapa ‘Man City’ hawakuamini jezi mpya zilipotambulishwa Septemba mwaka jana. Zilikuwa za rangi ya machungwa na zambarau. Zilifanana sana na jezi za ugenini za Barcelona.

Inasemekana moja kati ya sababu zilizomfanya Guardiola kukubali kutua Man City, ni uhakika wake wa kuhamia na watu wake anaowaamini.

“Lakini mfumo uliopo ni kama vile hatashindwa. Itakuwaje akishindwa? Itakuwa ni sawa na (Man City) kuanza upya,”  kilisema chanzo hicho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -