Sunday, October 25, 2020

Guardiola na mwanzo wa kuvutia ndani ya Man City

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

MANCHESTER, England

ALIPOTUA Manchester, macho na masikio ya wadau wengi wa soka walisubiri kumwona akidhihirisha ubora wake katika suala zima la ufundishaji soka tangu alipoanza na Barcelona hadi kuelekea Bayern Munich.

Na sasa akiwa na kikosi cha Manchester City, Pep Guardiola anafurahia kuanza kwa kasi ya hali ya juu iliyomfanya awe na mwanzo mzuri zaidi ndani ya viunga vya jiji La Manchester.

City imefikisha ushindi wa michezo nane tangu Mhispania huyo achukue mikoba ya kukinoa kikosi hicho na kufunga jumla ya mabao 25, huku ikiruhusu mabao manne tu. Mtanange wa mwisho waliichapa Bournemouth mabao 4-0 kwenye Ligi Kuu England.

Mpaka sasa City imeshinda michezo mitano ya ligi, wakiwa na pointi 15 kileleni mwa msimamo, huku wakianza vizuri harakati zao za kulisaka taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach, baada ya kuifunga Steaua Bucharest nyumbani na ugenini katika michezo yao ya kusaka nafasi ya kufuzu kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo miezi michache iliyopita.

Guardiola hajawahi kufikisha mechi tano za awali za ligi kwa timu yake kufunga mabao mengi na kuruhusu machache.

Katika mchezo wake wa kwanza wa German Super Cup akiwa na Bayern Munich ya Ujerumani, Guardiola alikutana na kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa Borussia Dortmund, iliyokuwa ikinolewa na Jurgen Klopp.

Katika michezo nane ya awali ya Bundesliga msimu huo wa 2013/14 dhidi ya Freiburg, Guardiola alijikuta akibanwa mbavu na Bayern yake kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo huo wa kwanza wa ligi, kabla ya kushinda michezo sita, ukiwemo wa kuwania UEFA Super Cup dhidi ya Chelsea, iliyokuwa ikinolewa na Jose Mourinho.

Mechi zake za awali akiwa na Barcelona msimu wa 2008/09 nazo hazikuwa nzuri sana akiwa kama kocha.

Alianza kuichapa Wisla Krakow mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza wa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kabla ya kuchapwa mchezo wa marudiano bao 1-0. Kikafuatia kichapo kingine kama hicho kwenye mchezo wa ufunguzi wa La Liga dhidi ya timu ndogo ya Numancia na sare ya 1-1 dhidi ya Racing de Santander, kabla ya kuibuka na ushindi kwenye michezo yao minne iliyofuatia.

Ushindi huo wa michezo minne uliendelezwa kwa kukusanya pointi tatu katika mechi 11 mfululizo za ligi na kuwafanya Barcelona kunyakua mataji ya La Liga, Copa del Rey na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ni mapema mno kuzungumzia suala la mataji ndani ya kikosi cha Manchester City kwa sasa, lakini wameanza vizuri mno chini ya utawala mpya wa Guardiola.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -