Sunday, January 17, 2021

GWIJI WA ENGLAND ATOBOA SIRI YA KULAWITIWA NA KOCHA WA VIJANA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

MOJA ya jambo gumu kwa mwanadamu ni kushindwa kuweka wazi kitu kibaya alichowahi kufanyiwa kwa hofu ya kwamba jamii itamchukuliaje, lakini mchezaji wa zamani wa England, Paul Stewart, ameamua kufunguka namna alivyodhalilishwa kijinsia na kocha wake wa timu ya vijana wakati akiwa mdogo.

Nyota huyo wa zamani wa klabu za Man City, Spurs na Liverpool mwenye umri wa miaka 52, alisema kocha huyo alimfanyia kitendo hicho kwa muda wa miaka minne baada ya kuwaahidi wazazi wake kuwa atamfanya awe maarufu kwenye soka.

Kwa zaidi ya miaka 40, Stewart alifanya jambo hilo kuwa siri, hata kwa familia yake kwani kocha huyo alimtishia kuwaua ndugu zake iwapo angefungua kinywa chake.

Lakini ameamua kutoboa siri ya namna kocha huyo alivyokuwa akimfanyia kitendo hicho kiovu alipokuwa na miaka 11 hadi 15, akiwa na matumaini ya wahanga wengine kujitokeza mbele ya jamii na kuzungumza baada ya kuiona habari ya mchezaji Andy Woodward, 43, aliyewahi kufanyiwa vitendo hivyo na kocha wa timu ya vijana ya Crewe Alexander, Barry Bennell, 61, katika miaka ya 1970 na 1980.

Stewart anaamini wapo wengine ambao waliwahi kufanyiwa vitendo hivyo kwa madai ya kuwepo kwa kundi kubwa la watu waliokuwa wakiendekeza mambo hayo Kaskazini Magharibi mwa England kwa muda huo.

“Kuna siku tulikuwa tunasafiri, akaanza kunishika shika. Niliogopa mno na sikujua nini cha kufanya, nilijaribu kuwaambia wazazi wangu wasimuite tena lakini ilishindikana kwa sababu ya umri wangu kuwa mdogo.

“Kuanzia hapo akaanza udhalilishaji, akanitishia kuwaua mama, baba na kaka zangu wawili kama nikisema chochote. Na kwa umri wa miaka 11 lazima uamini,” alisema.

Atumia dawa za kulevya kupunguza mawazo

Alipokuwa kwenye ubora wake wa kucheza soka, akipata fedha ya kutosha, bado alijiingiza kwenye dawa za kulevya ili kukata mawazo ya kudhalilishwa udogoni na aliamini ipo siku atasahau.

“Mawazo ya kujiua yalinijia kila wakati, hata nilipokuwa na kiwango cha hali ya juu ndani ya Spurs na England,” alisema.

“Giza lilitanda mno maishani mwangu na nilihitaji kutoka humo. Pombe ndio ilikuwa dawa kwangu. Kuna wakati nilijihisi mpweke, hata nilipokuwa nasakata soka.

“Nilianza kunywa sana pombe, nilikunywa sana hadi nilipoacha kuwaza. Nikaingia kwenye dawa za kulevya na nikazipenda kwani zilinipunguzia mawazo mno. Hapo ni wakati nikiwa na miaka 27 au 28.

“Dawa za kulevya nilizipata wakati wowote na mahali popote pale kila nilipohitaji. Sifahamu nilicheza kwa kiwango cha hali gani uwanjani. Lakini ndio uamuzi niliouchukua,” alisema.

Asifiwa na mkewe kwa kutoboa siri

Mke wake, Buv Stewart, ameonekana kufurahishwa na ujasiri wa mumewe kufunguka wazi juu ya kitendo hicho alichofanyiwa, kwani kitawasaidia na wahanga wengine ambao hadi sasa hawajaweza kujitokeza mbele ya jamii na kusema yote.

“Amefanya kitu sahihi. Nimefurahi mno kwa sababu amejiamini sana hadi kutamka wazi, sasa naweza kutembea bila aibu.

“Tuna watoto wa kike wawili na wa kiume mmoja wote bado wadogo, pamoja na watu wote wa familia tunajivunia mno juu yake,” alisema.

Bev na Stewart walikutana jijini Blackpool wakati mwanamke akiwa na umri wa miaka 19, na ndoa yao imedumu kwa miaka 29 licha ya mumewe kusumbuliwa sana na kumbukumbu ya kudhalilishwa iliyomfanya aingie kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

“Kwa wakati huyo nilihisi kitu. Wazazi wake waliniambia hakuwahi kusema kwa mwaka mmoja alipokuwa kijana mdogo, na nilimjua mwanaume aliyemfanyia udhalilishaji.

“Nilimuwaza sana huyo mtu aliyefanya kitendo hicho kwa mume wangu, japo yeye mwenye Paul hakuwahi kuniambia wazi.

“Sijui tulioana lini lakini hakutaka huyo mtu awepo eneo lolote karibu na sherehe yetu ya harusi.

“Ndipo kengele ikagonga kichwani mwangu. Hatukumwona tena baada ya hapo.”

Bev alisisitiza kuwa kitendo cha mumewe kuzungumza mbele ya jamii ni ‘jambo zuri’.

 

Historia yake:

*Amezaliwa Oktoba 7, 1964 jijini Manchester

*Nafasi: Mshambuliaji/Kiungo

*Alizichezea timu za Blackpool, Man City, Spurs, Liverpool, Crystal Palace, Wolverhampton, Burnley, Sunderland, Stoke City na Workington.

*Alifunga mabao 139 kwenye jumla ya mechi 559.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -