Wednesday, October 28, 2020

HABARI NDIYO HIYO…

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

HUSSEIN OMAR NA AYOUB HINJO

KAMA kuna anayedhani kikosi cha Simba kitakuwa na pengo kwa kumkosa nahodha wao, John Bocco, watakapocheza na Yanga Jumapili, basi atakuwa amepotea maboya.

Simba wanatarajia kuwa wenyeji wa Yanga keshokutwa Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku wakimkosa Bocco anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita walipovaana na Mwadui ya Shinyanga.

Kitendo cha kukosekana kwa Bocco katika mchezo huo, kimeonekana kupokewa kwa shangwe na watu wa Yanga wakiamini safu yao ya ulinzi itapumua.

Lakini, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ni kama amelibaini hilo la ‘kicheko’ cha watu wa Yanga na hivyo kuwafungia kazi ili kuwafunga mdomo kupitia nyota wa timu yake hiyo, Emmanuel Okwi.

Unajua ikoje? Ni hivi, Mbelgiji huyo ameamua kumkabidhi mikoba Okwi ili Mganda huyo aweze kuhakikisha anaisambaratisha Yanga keshokutwa.

Baada ya kumalizika kwa mazoezi ya Simba yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterans, Dar es Salaam juzi, Aussems, alionekana kuwa bega kwa bega na Okwi, huku wakiteta kwa sauti ya chini mambo kadha wa kadha kwa zaidi ya dakika 10.

Katika mazungumzo hayo, Bocco pia alijumuishwa na wote kuonekana kukubaliana baadhi ya mambo na mwishowe kupeana mikono.

Mpaka sasa Okwi hajafanikiwa kufunga bao lolote katika michezo miwili (dhidi ya Ndanda na Mbao) aliyocheza huku akiwakosa Mwadui alipoishia benchi, akiwapisha Meddie Kagere na Bocco waliofanikiwa kucheka na nyavu mara tatu.

Kwa jinsi ilivyoonekana juzi, Aussems, ana matumaini makubwa na Okwi kupeleka ‘msiba’ Jangwani kutokana na umahiri wake uwanjani, lakini pia uzoefu wake, hasa wakongwe hao wa soka nchini wanapokutana.

Ni kutokana na matumaini aliyonayo kwa timu yake, Aussems alipinga kikosi chake kwenda kuweka kambi Zanzibar au kwingineko kama ilivyozoeleka akidai ni kuwachosha wachezaji na kuwapa mzigo mkubwa kimawazo.

“Timu ilitoka Mtwara ikaenda Mwanza, halafu Shinyanga, lakini bado wanataka twende Zanzibar, ni kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa sasa.

“Wachezaji wanahitaji kupumzika kuliko kuwachosha kiakili na kuwapa mawazo, najua umuhimu wa mchezo huo ndio maana tunajiandaa kikamilifu kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Yanga,” alisema Aussems.

Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wamecheza mechi tano na kushinda tatu, suluhu moja na kupoteza mchezo mmoja, hivyo kujikusanyia pointi 10.

Kwa upande wao, Yanga wamecheza michezo minne na kushinda yote, hivyo kufikisha pointi 12.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -