Wednesday, October 28, 2020

‘Hakatwi mtu Simba’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

WAKATI kukiwa na taarifa za benchi la ufundi la Simba kutaka kufanya usajili wa wachezaji kadhaa wapya na kuwapunguza wachezaji walioshindwa kuonyesha kiwango bora kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi, Meneja wa kikosi hicho, Mussa Hassan ‘Mgosi’, amesema kuwa hawana mpango wa kumtaka yeyote.

Akizungumza na BINGWA, Mgosi alisema mara baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi, walikutana na benchi la ufundi na kuangalia mapungufu yaliojitokeza kuanzia mwanzao hadi mwisho wa mzunguko na kuona hawana haja ya kukibadili kikosi chao.

Alisema katika ripoti waliyoipeleka kwa uongozi, wameomba waongezewe wachezaji wachache ambao wataongeza nguvu katika kikosi, lakini pia kuwapa mikataba mipya wale waliomaliza kwa kuwa bado wanawahitaji.

“Hatuna mpango wa kumwacha mchezaji yeyote kwani wote wana umuhimu katika kikosi chetu, tunachokifanya hivi sasa ni kuongeza baadhi ya nafasi ambazo tunaona zimepwaya, lengo ni kukiimarisha kikosi chetu ili kiweze kutwaa ubingwa msimu huu.

“Ukiangalia kikosi chetu hakina mapungufu makubwa ya kutufanya tupunguze wachezaji, kwani kimejitosheleza na ni wazi kila mtu amekiona, hivyo basi suala la kuwapunguza halipo labda kama mchezaji ataamua kuondoka kwa utashi wake,” alisema.

Kikosi cha Simba kimeshinda michezo 11 na kupata sare mbili, huku wakipoteza mechi mbili katika mechi 15 walizocheza.

Kikosi hicho kilichopo chini ya  kocha Mcamerron, Joseph Omog, kinatarajia kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili Jumatatu ijayo baada ya kupumzika kwa wiki mbili, lakini kukiwa na tetesi kuwa huenda kikaenda kujificha nje ya Tanzania.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -