Sunday, October 25, 2020

HAKUNA TATIZO KUDHARAU KATIKA MAHUSIANO, MALIZA…

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

HAKUNA tatizo la kudharau katika mahusiano. Kila tatizo unatakiwa kulivalia njuga na kuhakikisha unalimaliza mapema, tena kabisa. Tatizo ni kama mimba. Kadiri unavyoiacha ndivyo inavyozidi kukua.

Mama mjamzito utakayekutana naye leo ni tofauti na mkikutana naye miezi minne baadaye. Ndivyo ilivyo pia katika matatizo. Tatizo unavyoliacha ndivyo linavyozidi kuwa kubwa na kutengeneza ugumu wa kulimaliza. Wengi walikuwa na uwezo wa kumaliza matatizo yao ila kwa kuyaacha leo yanawashinda.

Kama unaona mpenzi wako hayuko sawa katika baadhi ya mambo kwanini hutaki kumwambia? Kuna athari mbili kubwa za kuacha kumwambia ukweli mwenzako. Moja ni kwamba unakosa uhuru mwenyewe ndani ya nafsi, ila nyingine unafanya tatizo husika kuzidi kujenga mizizi.

Ni kweli wakati mwingine mambo madogo madogo ni ya kuyadharau ila hayafai kuwa yale yanayokunyima uhuru kwa kiwango f’lani. Unapoamua kutomwambia mwenzako kwazo alilokufanyia unajiweka katika hali ya kumuangalia mwenzako katika mtazamo tofauti.

Kiuhalisia utakuwa ukimtazama katika jicho la mtu mkosefu aliyetibua amani katika moyo wako. Katika mtazamo huu si mara zote utakuwa ukijiona uko katika mahusiano sahihi.

Wakati wewe utakuwa ukimtazama mwenzako katika hali hiyo, labda tena mwenzako atazidi kukukera kwa kurudia kosa kwa maana hajui kama unakereka. Atajua vipi wakati alipokosea hukutaka kumwambia?

Kuendelea kurundika makosa ya mwenzako ni njia ya kuja kuua mahusiano yako. Maana ipo siku utachoka na kuamua kumwambia jumla ya makosa yake yote, hapo ndipo kwenye tatizo kubwa.

Wakati unamueleza utamuona kama mtu asiyejali hisia zako vile. Kama mtu asiye na huruma na wewe hivi. Hapo  ndipo unaweza kujikuta unapandisha hasira kwa kuona huthaminiki mbele yake.

Kwa kufikiria makosa yote aliyokutendea unaweza kumuona kama ni mtu asiye na hisia na wewe na mwenye kupenda wewe uugulie kero zake. Kama binaadamu anaweza kutokubali na kuona unamuonea.

Kwanini asione unamuonea ikiwa hukuwa unamwambia? Kwanini asione unamtafutia sababu tu wakati ulikua ukiyamezea? Hawezi kukubali kirahisi.

Anaweza kujikuta akikujibisha hovyo kwa kuona unamuonea. Katika hali kama hii suluhisho kupatikana haiwezekani, kwa maana huwezi kumuona yuko sahihi hata kidogo. Akukosee, akukaripie alafu bado umuone yuko sahihi? Haiwezekani!

Maneno ya kashfa, dharau na masimango yanaweza kuchukua nafasi yake hapo! Kitakachotokea hata wewe unaweza kutabiri.

Balaa lote hilo limesababishwa na kukumbatia kosa hata kama linakuumiza. Maisha hayaendi hivyo wala wapendanao hawawezi kudumu kwa  mtindo huo. Ikiwa unaona kuna tatizo kwa mpenzi wako ni suala la kukaa pamoja na kulimaliza. Usikae wala kungoja mpaka ajue mwenyewe- hapana.

Bora hata umwambie kwa kutumia njia nyingine lakini si kukaa kusubiri ‘lijisolve’ lenyewe, hapana. Matatizo yanapokuwa mengi hata utatuzi wake unakuwa mgumu. Ukiacha kumwambia mwenzako juu ya makosa anayokufanyia jua hata hukumu utakayotoa dhidi yake haina tofauti na uonevu.

Unamhukumu siku unayomwambia makosa yake? Uliona wapi hiyo? Ili kujua kama anakufanyia makusudi ama anapitiwa ni vyema akajua wapi anakukwaza.

Mwingine kutokana na mazingira aliyokulia haoni kama anakukwaza kuwa na ukaribu na wenye jinsia tofauti na yake. Ukiacha kumwambia jua ataendelea kuwa hivyo bila kujua kama anakukwaza. Suala ni kumwambia tu – ukimwambia na bado akafanya hivyo hapo ni habari nyingine. Haitakuwa vibaya kumfikiria tofauti.

Ila si sasa, katika hali hii ya kumezea unachokosewa. Kosa haliwi kosa kama mhusika hajui kama alilofanya ni kosa. Mwambie kosa hivi ili akirudia tumuone ni mkosaji.

ramadhanimasenga@yahoo.com 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -