Thursday, December 3, 2020

Hakuna ugomvi usio na suluhu kwa wapenzi wakiamua

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

USIJARIBU kutoa maamuzi ya haraka ya kuwataka kuachana ukiona wapendanao wako katika uhasama. Hisia za mapenzi baina ya watu wawili wanaopendana huwezi kuzipima kwa haraka haraka.

Wengine wanapogombana sana wewe unadhani kuwa wamechokana, kumbe wanapendana sana ndiyo maana jambo dogo linaleta shida kwao, kwa sababu ya hisia kali za kiwivu baina yao.

Hata ukiona mmoja kamsaliti mwenzake na mwingine akagundua, usiwe kiherehere kutaka waachane. Wenyewe wakikaa watayamaliza na kisha utajiona huna nafasi tena. Mdundo wa mapenzi hauchezwi na mtu mwingine ila wale tu walio katika mahusiano husika.

Usione wanapigana hadharani ukadhani ndiyo tamati ya umoja wao wa kihisia, wakiingia ndani  watayamaliza kwa namna ambayo huwezi kuamini. Mapenzi ni ya wawili.

Mwingine ukitaka kuingia na kujifanya yanakuhusu sana kuliko wahusika wenyewe, kitakachotokea mbele yake unaweza kujiona umewahi kuwa mjinga sana.

Angalia Bill Clinton na mke wake, Hilary, kila kitu kilikuwa wazi juu ya mahusiano ya Clinton na yule mfanyakazi wa Ikulu, Monica Lewinsky. Ukimya wa Hilary mwanzo ukawapa watu tafsiri ya kuamini kuwa mwanamama alikuwa anapanga mikakati ya kumbwaga mheshimiwa. Ila nini kilitokea baadaye?

Hilary badala ya kuwa mtu wa kumlaumu ama kumkashifu Clinton kutoka na mfanyakazi wake wa Ikulu kama ilivyoaminiwa na wengi, yeye akageuka kuwa mtetezi wa mume wake. Akapinga kila tusi alilotukanwa mumewe, akapinga hata kuwahi kuwa na uhasama na mumewe kutokana na kashfa hiyo.

Kumbe kipindi kile alipokuwa kimya hakuwa anawaza namna gani anaweza kuachana na mumewe, ila kumbe alikuwa anawaza ni kwa namna gani anaweza kuendelea na mumewe pamoja na kufanyiwa usaliti mkubwa na dunia nzima kujua. Ugomvi wa wapendanao usijifanye kuwa shahidi namba moja.

Wapenzi wenyewe wanajuana. Wapenzi wenyewe wanafahamu kila mmoja ana thamani gani kwa mwenziwe kimaisha. Wapenzi wa kweli kuachana si chaguo la kwanza.

Huwa kwanza wanaangalia thamani yao wawili. Je, wanafurahishana, wanaheshimiana, mipango yao ya kuwa pamoja kimaisha inatoa picha nzuri? Wakiwaza haya hata mmoja akapitiwa na ‘ushetani’ na kufanya ujinga, ugomvi wao huzungumzika.

Wao upamoja wao huwa na thamani zaidi kuliko utengano wao bila kujali kosa. Wao kusameheana huwa rahisi sana kutokana na ukubwa wa hisia zao kwa kila mmoja.

Ukiona wapenzi wanagombana na wanakutaka ushauri, acha kukimbilia kuangalia nani kakosea nini. Badala yake angalia ni kwa namna gani wanaweza kusahau mapitio yao na kuendelea na maisha yao.

Hakuna ugomvi usioweza kusameheka kwa wapenzi. Hata iwe vipi, ila kama kila mmoja katota kihisia kwa mwingine kila kitu huwa rahisi.

Kwani hujawahi kusikia mtu aliwahi kumfumania mwandani wake na kisha baadaye wakasahau na kuendelea kuwa pamoja? Huwa sio uchawi, huwa sio mauzauza, hayo huitwa mapenzi ya ndani. Mapenzi ambayo kwa jicho la kukurupuka huwezi kuyaona asilani.

Nini kinashindikana katika mapenzi?

Kama mtu anaweza kubadili dini na kuolewa, kama mtu anaweza kuhama nchi na kuoa ughaibuni, kama mtu anaweza kuwa radhi kugombana na ndugu  na marafiki zake kwa ajili ya fulani, sasa kosa gani gumu katika mapenzi lisilostahili msamaha?

Mapenzi ya mmoja na mwingine huwezi kuyapima kwa akili na muono wako. Mapenzi yao wenyewe yanapimwa na hisia zao wenyewe.

Kwa sababu ni kwa hisia hizo ndipo waliporidhiana na kwa hisia hizo hizo ndipo wataachana kama ikibidi kuwa hivyo.

Jidanganye kuwa unaweza kupima upendo wa mwingine kupitia macho na ushawishi wako.

Wengine walilazimishwa kwa namna yoyote kuachana na machaguo yao na kwenda kwa machaguo ya wazazi ama marafiki zao. Wengine bila kupenda ama baada ya kurubuniwa na tunu za dunia walikubali, ila unajua kilichotokea baadaye?

Wengine tayari wamerudi kwa wapenzi wao wa mwanzo, baadhi japo wako katika mapenzi na wahusika mpaka leo ila bado wanakutana ‘michezoni’ na wapenzi wao wa zamani. Kama unaamini una akili timamu acha kujidanganya kupima upendo wa watu kwa macho.

Wewe jiaminishe tu kuwa yule anajifanya anampenda sana mume wake ila kwa utajiri wangu ni lazima nimng’oe. Jidanganye kisha mfuate. Unaweza kumng’oa sawa, ila usiamini furaha iliyopo katika mahusiano yao itahamia na kuja kwako, hapana.

Atakuwa nawe, atalala na wewe ila sio kwa furaha na amani kama ilivyokuwa na yule jamaa wake. Atasema anakupenda ila si kwa dhati na kwa bashasha, utampigia simu atapokea ila abadani hatokuwa na shauku ya simu yako kama ilivyokuwa kwa yule jamaa wake.

Ila na mbaya zaidi ile thamani ya mapenzi, ile hali ya upekee ambayo kila mmoja anaitamani kwa mwenzie haitokuwa kwako. Atasema anakupenda ila atakwenda ‘michezoni’ na yule mwingine ama na hata wengine.

Atafanya hivyo kwa sababu hana ile kitu  inaitwa ‘Moral respect’ kwako. Akuheshimu ama akujali vipi wakati hakuhisi ndani ya nafsi yake?

Waone wale wanavyopendana kila mmoja anaonekana ana furaha, waone wanavyocheza pamoja ila usijaribu kupima uhusiano wao kwa macho yako. Wengine wanaonekana kupendana na walio nao ila kimsingi wanaigiziana.

Wengine wanatoka katika majumba makubwa na kila mwisho wa juma wanatoka kwenda katika mahoteli ya kifahari, ila kumbe mmoja kati yao analazimika kufanya tu ilimradi, ila hana hisia wala shauku ya kweli kuwa na mwenzake.

Unaona wale wanavyopendana, unaona wanavyocheka pamoja, ila acha kuhukumu uhusiano wao kwa akili yako. Wengine wako hivyo sio kwa sababu ya mapenzi, ila wako hivyo kwa sababu ya kibiashara. Biashara gani? Sijui!

 ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -