Friday, December 4, 2020

HALI YA MTOTO BRADLEY SI NZURI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

MTOTO anayesumbuliwa na kansa, Bradley Lowery, hali yake imezidi kuwa mbaya akiwa hospitalini kiasi cha kuahirisha ziara ya ‘rafiki yake’ Jermain Defoe aliyekuwa anatarajiwa kumtembelea mtoto huyo mapema wiki hii.

Picha iliyowekwa kwenye mtandao wa Daily Mail, ilimuonesha Lowery akiwa amelala kitandani hajiwezi, huku mrija ukiwa umechomekwa kifuani mwake na uso wake ukionesha huzuni.

Mapema wiki hii, dogo huyo alikuwa akitabasamu vilivyo baada ya kugundua kuwa angeenda kuwa mmoja wa watoto waliotakiwa kuongozana na wachezaji wa timu ya Taifa ya England katika mchezo wa kufuzu kushiriki Kombe la Dunia, ambapo pia rafiki yake, Defoe aliitwa kucheza mchezo huo.

Video iliyomwonesha akifurahia kuongozana na Defoe ilitupiwa kwenye ukurasa wake maalumu wa Twitter, ikisindikizwa na maneno: “Bradley alifurahi mno kusikia Defoe kaitwa kuichezea England.”

Kipande hicho kilimuonesha Bradley akiwa amekaa kwenye kiti, huku sauti ya mama yake Gemma ikisikika akimuuliza: “Otea. Otea nani atakuwepo kwenye mechi ya England wiki ijayo?”

Bradley akauliza: “Nani?”

Gemma akamjibu: “Jermain.”  Jibu lililomfanya Bradley arukeruke kwa furaha.

Urafiki wa Bradley na Defoe ulianza kushika kasi katika miezi ya hivi karibuni, baada ya dogo huyo kukumbwa na mtihani wa kupambana na kansa inayofahamika kitaalamu kama ‘neuroblastoma’ kwa mara ya pili.

Mwezi uliopita, Bradley alianza kuonekana akiwa na Defoe, hasa kwenye mechi za Sunderland baada ya familia yake kuripoti kansa mpya iliyoanza kumwandama, ambapo majibu ya uchunguzi yalionesha kansa hiyo ilivamia mgongoni mwake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -