Thursday, December 3, 2020

HANS PLUIJM ALITIMULIWA YANGA ZAMANI SANA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA OSCAR OSCAR

KINACHOENDELEA kwa sasa ndani ya Klabu ya Yanga, hakina tofauti kubwa sana na kile kinachoendelea ndani ya Klabu ya Barcelona. Hapa kocha Loius Enrique Martinez, pale Hans van der Pluijm. Baada ya kushinda mataji makubwa matatu katika msimu wake wa kwanza (La Liga, Klabu Bingwa Ulaya na Kombe la Mfalme) na kushinda mawili msimu wake wa pili (La liga na Kombe la Mfalme), inashangaza kusikia Barcelona haimhitaji tena kocha wake, Martinez.

Baada ya kushinda mataji mawili mfululizo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la FA (Azam Sports Federation) na kuiongoza Yanga kutinga hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, unashangaa kuona Yanga haimhitaji tena kocha wao, Pluijm!

Hii ndiyo akili ya mwanadamu anapohitaji lake, usimwamini sana mwanadamu anapohitaji lake. Mwishoni mwa juma lililopita, Yanga walitangaza rasmi kuachana na Mkurugenzi wao wa ufundi, Hans van der Pluijm.

Taarifa hii wala haikuwa mpya kwenye ngoma za masikio yangu, kwa sababu naamini Mdachi huyo alishaondoka Yanga tangu alipoondolewa kwenye nafasi yake kama kocha mkuu wa klabu hiyo. Baada ya ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Sporting Gijon katikati mwa juma lililopita, kocha Loius Enrique Martinez alitangaza kuwa hatakuwa na Barcelona tena baada ya msimu huu.

Hii pia haikuwa habari mpya kwanza kwa sababu Barcelona haijaonyesha kama inamhitaji kocha huyo tena. Haiwezekani mpaka anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake klabu ikawa kimya. Hii ilikuwa ni ishara tosha kwamba safari ya Martinez ndani ya Catalunia imefika mwisho.

Siamini kama Yanga wameachana na Hans juzi. Hawa watu walichokifanya ni kutuliza tu mzuka wa mashabiki ambao walionekana kutokubaliana tangu awali kwa kumwondoa Pluijm kwenye nafasi ya ukocha na kumleta George Lwandamina.

Waliwatuliza mashabiki kwa kuwaambia kwamba Pluijm atakuwa Mkurugenzi wa ufundi lakini kiuhalisia shughuli ya Hans na Yanga ilimalizika siku nyingi sana. Si jambo geni wanalofanya Yanga, mwanadamu yuko hivyo kiasili. Kuna muda anahitaji mabadiliko na hakuna wa kumzuia. Yanga wanahitaji mabadiliko, hakuna wa kuwazuia. Barcelona wanahitaji mabadiliko na hakuna wa kuwazuia.

Hawa ni makocha wanaoondoka ndani ya klabu zao kwa sababu ambazo hata mtoto mdogo hawezi kuziamini. Wapo watu wanaoamini kwamba Martinez hana jipya tena na hana uwezo mkubwa wa kufanya usajili wenye tija. Watu hawa wanasahau kwamba pamoja na usajili wake wa Dennis Suarez, Samuel Umtiti na Lucas Digne kushindwa kufikia lengo msimu huu, bado hawa wote ni vijana wadogo na hakuna hata mmoja anayezidi umri wa mika 23.

Lakini pia, ni huyu huyu Martinez aliyemsajili Luiz Suarez na Ivan Rakitic ambao ni sehemu ya kikosi cha kwanza cha Barcelona. Kiufupi, hakuna hoja ya msingi ya kumwondoa Martinez. Baada ya kutwaa kila taji la ndani waliloshiriki Yanga msimu uliopita na kutinga hatua ya robo fainali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, hakukuwa kabisa na sababu ya msingi ya kumwondoa kocha Hans lakini huyo ndiyo mwanadamu.

Baada ya Hans, maisha lazima yaendelee ndani ya Yanga kama ambavyo mambo yatakavyoendelea ndani ya Barcelona baada ya Martinez. Hans amefanya makubwa ndani ya Yanga kwenye kipindi chake, naamini mchango wako utakumbukwa daima kama ambavyo Martinez alivyoifanya Barcelona kuwa tishio kwenye idara ya ushambuaji kuwa kutokea baada ya kuwasuka Lionel Messi, Neymar na Luiz Suarez na kufanikiwa kuvuna mataji.

Hawa ni makocha wawili wanaoondoka kama wafalme ndani ya klabu zao kwa sababu za kibinadamu tu. Pamoja na yote, bado naamini Camp Nou pataendelea kuwa nyumbani kwa Enrique Martinez kama ambavyo Jangwani patakavyobakia kwa Hans Pluijm.

Nina imani kubwa kwamba milango ya kocha Hans siku zote itaendelea kuwa wazi pindi Wanajagwani hao watakapomhitaji kama ambavyo Martinez atakavyoipokea Barcelona. Pluijm hakufukuzwa juzi Yanga, ni muda mrefu sana tangu alipoondolewa kwenye nafasi ya kuwa kocha mkuu. Huku kwenye ukurugenzi wa ufundi ilikuwa ni danganya toto tu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -