Wednesday, October 28, 2020

Hans Pluijm amng’ata sikio Lwandamina

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA

HANS van der Pluijm amejichimbia kuandaa ripoti ambayo ndiyo hasa itakayomsaidia mbadala wake, George Lwandamina, katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingineyo ijayo.

Lwandamina, ambaye amepewa kazi maalumu ya kuhakikisha Yanga inafanya vema kwenye ligi na mashindano ya kimataifa, ameanza kuangalia kikosi hicho kwenye mikanda mbalimbali ya video.

Habari za ndani ambazo BINGWA imezipata, zinasema Lwandamina ameanza kukusanyiwa mikanda hiyo tangu alipowasili Dar es Salaam, ambapo hadi sasa inasemekana nyota wawili wa timu hiyo, wamekalia kuti kavu.

Wakati Lwandamina akiendelea na yake, Pluijm naye amejifungia akiandaa ripoti ya mzunguko wa kwanza, lakini pia itakayokuwa na matukio yote aliyokabiliana nayo tangu aliporejea Yanga kwa mara ya pili.

Kocha huyo raia wa Uholanzi, alipozungumza na BINGWA jana, alikiri juu ya hilo la kuandaa ripoti ambayo ataiwakilisha kwa uongozi wa Yanga, ili iweze kufanyiwa kazi na Lwandamina.

Pluijm aliliambia BINGWA jana jioni: “Bado nipo sijaondoka, nipo ‘bize’ sana nikiandaa ripoti yangu.”

Japo Pluijm hajaweka wazi, lakini inafahamika kuwa katika ripoti yake hiyo, kutakuwa na mapendekezo yake juu ya wachezaji gani wa kuachwa na sababu za kufanya hivyo, lakini pia wale anaodhani wakisajiliwa wanaweza kuibeba Yanga mzunguko wa pili na kwenye mechi za michuano ya kimataifa.

Tayari wachezaji wanaodaiwa kupendekezwa kutemwa Yanga ni Mbuyu Twite na Obrey Chirwa, huku nyota wengine wazawa wakiwa kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo.

Kwa upande wa wanaotarajiwa kusajiliwa Yanga, ni kiungo Mzambia, Meshack Chaila na Mkenya Jesse Were, ambao ni wachezaji tegemeo katika kikosi cha Zesco ya Zambia, iliyokuwa ikinolewa na Lwandamina na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -