Friday, December 4, 2020

HAPA NDIPO MAHALI PA KUONESHA UPENDO WAKO

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

KUNA mahali ambapo upendo wako kwa muhusika unapoonekana. Si  katika hayo matumizi wala katika ahadi unazompa. Kama una hela matumizi kitu gani? Kama una uwezo wa kuongea unashindwa vipi kutoa ahadi?

Ndiyo, ni mambo ambayo kwa namna fulani yanaonesha kujali kwako ila bado. Kuna mahali fulani hivi. Kama ukifanya kitu au kutenda jambo, hata wewe unahisi bila upendo wako na kumuhitaji kwako katika maisha, usingeweza kufanya hivyo. Si kitandani wala sebuleni. Kuna  mahali hivi.

Japo kuna mambo kadha wa kadha yanaweza kuwa yametokea ila kwa sababu ya upendo wako kwake utafanya jambo fulani. Jambo kubwa katika kuonesha ni kwa namna gani alivyo na thamani na umuhimu katika maisha yako. Si katika manunuzi ya vitu vikubwa wala kumjengea nyumba. Upendo wako uko mahala pale. Pale  utakapofanya kitu, kwa wengine kigumu kufanyika ila kwako unafanya.

Si kwa shinikizo wala amri ya mtu, ila ni kwa ajili ya thamani na umuhimu wa fulani katika maisha yako. Umewahi kufikiria katika suala la kutoa msamaha kwa upana wake?

Kwa makosa yake bila kujali kama yalikuwa makubwa au madogo ila unaamua kumsamehe. Wengine wanaweza kusema hili na wengine wakapakaza lile, ila kwa dhati ya nafsi yako unaamua kumsamehe na kuamua kufungua ukurasa mwingine katika maisha yako. Si suala dogo. Ni suala linaloonesha namna unavyopenda na kujali.

Kumsamehe mtu maana yake unataka kufuta yaliyotokea na kuangalia mengine. Ni wapi unapoweza kuziba upendo wa namna hii? Japo kakuumiza, ulimwambia hili akafanya vile, ila kwa kuwa unamuhitaji unaamua kumsamehe. Ni hapa unapoweza kujiangalia na kugundua fulani alivyojaa katika moyo wako na kuongelea katika akili yako.

Msamaha ni moja ya nguzo kubwa za kuonesha thamani ya fulani katika maisha yako. Ndiyo, kakosea, alikuuliza hata kukufanya kujihisi mnyonge ila kwa kuwa katubia kwa dhati na kuahidi kufanya mengi  mazuri unaamua kumpokea tena katika bustani yako ya upendo. Ni upi upendo kama si huu?

Baadhi huwa na tafsiri hasi juu ya suala hili.Wakiona wenzao wametoa msamaha kwa wapendwa wao, hudai fulani ni zoba, sijui mjinga na kwanini kamsamehe. Kamsamehe kwa kuwa anaona umuhimu katika maisha yake.

Anamsamehe kwa kuwa katubia kwa dhati na kujua anampeda sana mwenzake, sasa kama wanapendana wasisahau yaliyopita? Tena wakiwa wameahidiana kuishi kwa amani na furaha zaidi ya mwanzo? Kuna vitu vingi unaweza kufanya kuonesha namna unavyomjali na kumpenda mwenzako. Unaweza  kumpa zawadi, kuwa mwema sana kwake, kumjali na kumthamini kwa kila namna, ila unaweza kuonesha umuhimu wake katika maisha yako kupitia msamaha. Kama  humsamei ina maana uko radhi aondoke na kwenda kuangalia maisha mengine. Ila kama unamsamehe je?

Najua kuna baadhi ya watu hawatakiwi kusamehewa. Kama wanafanya makosa na bado kuona ni sahihi wao kufanya hivyo, msamaha si kitu wanachotakiwa kukipata. Msamaha ni kitu mahsusi kwa ajili ya mtu anayejali na kuthamini.Hata baada ya kukufanyia makosa, akakufanya pengine ulie ila kwa kuwa ameona kosa lake.Akalilia na kuomba kwa dhati msamaha, inafaa asamehewe.

Msamaha kwa mtu anayejali na kuthamini ni kipimo cha kujua ni kwa namna gani unavyomuhitaji mwenzako. Kuna watu wanaachana kwa kosa hata la kuchelewa kupokea simu kwa dakika moja. Wengine wanaachana kwa sababu tu leo kapitia njia hii na si ile. Hawaombani masamaha na hawajutii kuachana. Unajua kwanini?

Katika nafsi zao kuna kitu wanakosa. Hisia za dhati na hekima ya penzi hawana. Sasa kwanini waombane msamaha na kwanini wasiachane? Msamaha maana yake unajali na kuthamini uwepo wa mwenzako katika maisha yako. Unajali na kuona akiondoka ataondoka na kitu katika maisha yako. Huenda ni furaha au tumaini au ikawa vyote kwa pamoja. Nani anataka kukosa vitu hivi. Kuna mengi unaweza kufanya kwa mpenzi wako kuonesha unampenda, ila kusamehe ni hali mwafaka katika kuonesha umuhimu wake katika maisha yako.

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -