Friday, November 27, 2020

HARMORAPA HUITAJI TENA KIKI, FANYA KAZI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR,

KIKI si kitu kigeni kwa wasanii popote duniani na maana halisi ya neno hili ni kutafuta jambo la kushtukiza kuwafanya mashabiki kumzungumzia msanii husika kwa muda mrefu zaidi.

Kiki hutumika kutafuta zaidi kuongelewa zaidi kwenye televisheni, redio na kwenye mitandao ya kijamii ambako wasanii wamekuwa wakitafuta njia hii ili kusaidia kazi zao kusikilizwa zaidi.

Kwa kawaida kiki ni nzuri na humsaidia msanii kumpandisha kiwango ambapo kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la wasanii kutengeneza stori ambayo itawafanya watu kuwa makini katika mitandao ya kijamii ili tu azungumziwe sana.

Wapo mastaa mbalimbali Bongo ambao wametingisha kwa kiki na kufanya wazungumziwe sana na matokeo yake kupata faida ya kufanya promo kwa kazi wanazozifanya.

Hivi karibuni ameibuka msanii aliyejiita Athumani Omary ‘Harmorapa’ akiwa anafanana sana na mwanamuziki, Rajabu Abduli ‘Harmonize’, aliyechini ya lebo ya WCB.

Hakuna aliyekuwa anamjua Harmorapa hapo awali, lakini kiki zake za kila kukicha zimewafanya kila mtu kumtolea macho kumwangalia msanii huyo ambaye tayari ametoa wimbo wake unaojulikana kwa jina la Usigawe Pasi.

Alianza kama utani vile na kiki ya kufananishwa na Harmonize ambapo hapo alipachikwa jina la ‘kiboko ya mabishoo’ jina ambalo linaendelea kumbeba kila kukicha.

Harmorapa akaja na staili nyingine ya kumpigia goti msanii Ali Kiba, alipoibuka kwenye mapokezi yake pale Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) alipokuwa anawasili kutoka Afrika Kusini alipotoka kuchukua tuzo ya MTV.

Alipofanya tukio hilo jina lake lilizidi kujaa masikioni mwa mashabiki mbalimbali wa burudani na wengi walimtaja kama msanii aliyeingilia bifu la Ali Kiba na Nassib Abdul ‘Diamond’.

Harmorapa aliendelea kutafuta kiki baada ya kuweka video kwenye kurasa zake mbalimbali akionyesha kuwa na fedha nyingi ambazo baadaye zilitajwa kuwa ni za meneja wake.

Tukio ambalo wengi hawakulitarajia ni msanii huyo kuonekana kwenye ofisi za Clouds Fm eti akitoa pole baada ya watangazaji wake kushikiwa bastola kwenye tukio lililotokea mwezi huu.

Achana na pole, mbio alizozoka wakati wa tukio la kuonyeshwa bastola kwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, limemfanya jina lake kuendelea kuwamo kwa mashabiki wake mbalimbali.

Staili nyingine aliyoingia nayo kama gia ni ‘kumtusi’ Moses Iyobo mpenzi wa Aunt Ezekiel kuwa mkata viuno hawezi kubishana naye jambo lililomfanya kupata mashabiki wengi zaidi wa kusikiliza wimbo wake wa Kiboko ya Mabishoo aliomshirikisha mkongwe, Juma Nature.

Lakini yote tisa kumi ni kitendo cha hivi karibuni cha Harmorapa pale alipoamua kuushangaza umma wa Watanzania kuwa ana uwezo wa kumuoa msanii mwenzake, Wema Sepetu na kumpangia nyumba kama haitoshi msanii huyo alijinadi kuwa ana mzigo wa kutosha wa kufanya jambo lolote kitu ambacho naweza kusema si sawa katika kipindi ambacho anatafuta njia ya kutokea.

Wengi walidhani kama utani pale alipoanza kiki ili kujitangaza, lakini kwa sasa amekuwa ndio stori ya mjini na kila mmoja hutamani kumsikia kila kukicha hivyo inampa unafuu kwenye kazi zake.

Binafsi ningependa kumshauri Harmorapa kujikita zaidi katika kuboresha kazi zake za kisaniii na kuachana na kiki ambazo hazina kichwa wala miguu na mwisho wa siku ataishia kuwaboa wasanii wenzake na mashabiki wake pia.

Umefika wakati sasa wa mashabiki wa Harmorapa na wadau wa muziki wa Bongo Fleva kusikia kazi za msanii huyo kwani ninaamini tayari wamechoshwa na matendo yake ya kutafuta kiki hivyo wana hamu ya kusikia nini anakiimba hivi sasa.

Ni wazi kwa kufanya hivyo kutamsaidia yeye kuongeza kipato chake lakini pia kumtangaza zaidi katika medani ya muziki wa Bongo Fleva badala ya kutumia kiki kuendeshea maisha yake.

Lakini pia Harmorapa lazima ukumbuke wakati ni ukuta, tayari umepata nafasi tengeneza nyimbo, fanya albamu kabla ya wadau wa Bongo Fleva hawajakuchoka kutokana na vitendo vyako vya kutafuta kiki ambazo hazina kichwa wala miguu.

Angalia wasanii wenzake akina Darasa, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Diamond, Ali Kiba, Dully Sykes, Abdul Kiba, Harmonize na wengineo walivyopiga hatua katika soko la muziki na kazi zao sasa zinasikika lakini pia wamefanikiwa kupata matangazo katika makampuni mbalimbali ya simu na watu binafsi kutangaza biashara zao na wao wameweza kujiongezea kipato kupitia matangazo hayo.

Fanya kazi sasa muda wa kupata kiki umekwisha, jali muda kabla haujakutupa mkono, kumbuka kuwa fainali uzeeni tengeneza maisha sasa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -