Saturday, August 15, 2020

HATA SPURS WATATWAA TAJI LA UEFA KABLA YA ARSENAL

Must Read

Mkwasa kocha mpya Ruvu Shooting

NA WINFRIDA MTOI ALIYEKUWA Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa amepata ajira ya kuinoa...

Simba ukuta wa chuma

NA WINFRIDA MTOI KLABU ya Simba imekamilisha safu yao ya ulinzi baada ya kumsajili...

Wakili kiboko anunua kesi ya Morrison

NA WINFRIDA MTOI WAKALI aliyejizolea umaarufu nchini kutokana na uwezo na rekodi yake ya...

NA OSCAR OSCAR

TUSIBISHANE kuhusu hili, uwezo wa mzee Arsene Wenger kujenga kikosi imara chenye ushindani umepungua kwa sasa. Sioni namna yoyote ya Arsenal kushinda taji la Klabu Bingwa Ulaya chini ya mzee Wenger.

Sioni pia dalili za kushinda taji la EPL na wasiwasi ninaouona ni Arsenal kumaliza nje ya nne bora kwa mara ya kwanza msimu huu tangu kocha huyo alipoichukua timu hiyo mwaka 1996. Usibishe, Arsenal inaweza kumaliza nje ya nne bora msimu huu.

Usibishe, Mesut Ozil na Alexies Sanchez wanaweza kuondoka baada ya msimu huu kumalizika. Arsenal imekuwa timu inayotegemea muuzija wa soka zaidi kuliko ubora walionao. Ni kweli bahati ipo kwenye mchezo wa soka lakini unahitaji pia kuwa na kikosi bora.

Jumatano iliyopita Arsenal wametoka kadhalilishwa na The Bavarians, Bayern Munich kwa kufungwa mabao 5-1. Matokeo haya ni mwendelezo wa kutonesha kidonda kwa mashabiki wa Arsenal ambayo wameishuhudia timu yao iking’olewa katika hatua ya 16 bora kwenye michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya kwa mara ya sita mfululizo.

Kibaya zaidi ni kwamba, hakuna anayejali. Kocha Arsene Wenger hajali, Mkurugenzi Mkuu, Ivan Gazidis, naye hana mpango. Ni kama ndoto za Arsenal kila mwaka ni kupata nafasi ya kushiriki Uefa basi. Kichapo walichopata Gunners dhidi ya Bayern Munich kwenye mechi ya kwanza, maana yake Arsenal anasubiri muujiza wa soka kuweza kupindua matokeo.

Timu itaishi kwa muuzija mapaka lini? Heshima ya Arsene Wenger ndani ya Arsenal itabaki pale pale kwa sababu yapo mengi mazuri waliofanya kwa klabu hiyo. Mataji matatu ya ligi kuu na yale sita ya FA ni sehemu ya mafanikio makubwa aliyofanikiwa Wenger ndani ya uwanja, lakini ataendelea kukumbukwa zaidi kwa kuimarisha uchumi wa Arsenal na hasa baada ya kufanikisha upatikanaji wa Dimba la Emirates. Pamoja na hayo yote, muda si rafiki wa Wenger.

Pamoja na kuwa Arsenal ndiyo timu kubwa na yenye mafanikio zaidi kutoka ndani ya Jiji la London, lakini haijawahi kushinda taji la Mabingwa Ulaya. Chelsea ambalo hapo awali walionekana ni timu ya kawaida, wameshatwaa taji hilo lenye heshima kubwa sana barani Ulaya.

Spurs wanaonekana wadogo kwa sasa lakini huenda watakuja kushinda taji la Ulaya kabla ya Arsenal. Mzee Wenger amekuwa anajenga kila siku kikosi ambacho hakina uwezo wa kupambana. Arsenal imeendelea kuwa mpya kila kukicha tofauti na kinachoendelea pale kwa majirani zao wa Spurs.

Pochettino ametengeneza kikosi kazi ambacho kwa sasa kinakosa uzoefu tu, ndani ya misimu miwili ijayo tunaweza kushuhudia Spurs ikitamba juu ya Arsenal. Unapotazama kizazi cha Spurs cha leo chenye watu kama Victory Wanyama, Delle Ali, Harry Kane, Christian Erikssen, unapata picha ya wafalme wapya wa London. Hii Spurs ikiongeza watu kama watatu tu wa aina ya James Rodriguez, Pieere Emerick Aubameyang na Vincent Kompany wanaweza kusumbua si EPL tu ni mpaka kwenye Uefa.

Tatizo la Arsenal halisababishwi na kocha pekee ni mpaka uongozi. Arsenal haina viongozi wenye kiu ya kushinda mataji ndiyo maana kila msimu wanafungua ‘shampeni’ kupongezana kwa kumaliza ndani ya nne bora kwenye msimamo wa ligi kuu. Uongozi mzima wa The Gunners na kocha Wenger ni kama pipa na mfuniko.

Lengo lao ni kutengeneza pesa kwa njia nyingine na si matokeo ya uwanjani na ndiyo maana pamoja na Arsenal kuendelea kuchemsha, lakini hana hata wasiwasi na kibarua chake. Kwa namna kocha Mouricio Pochettino anavyotengeneza kikosi chake, nashawishika kwamba Spurs wanaweza kushinda mataji ya EPL na Uefa kabla ya Arsenal.

Muda wa kocha Wenger umekwisha pale Arsenal, hakuna lolote kubwa atakaloendelea kufanya ndani ya uwanja. Angehamia kwenye uongozi na kuachia kijiti. Ni vema kulinda heshima yake kwa kujiweka pembeni. Akiondoka Mesut Ozil na Alexies Sanchez, Arsene Wenger atakuwa amemwachia mtihani mkubwa sana kocha atakayefuatia pale Emirates Stadium.

Grafu ya mzee Wenger inashuka kila kukicha, matumaini ya Arsenal kushinda taji lolote msimu huu nayo yanazidi kufifia. Wenger akiendelea kubaki, siku si nyingi atapoteza hata hiyo nafasi ya nne ambayo ndiyo imekuwa kama mafanikio yake ya kudumu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Mkwasa kocha mpya Ruvu Shooting

NA WINFRIDA MTOI ALIYEKUWA Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa amepata ajira ya kuinoa...

Simba ukuta wa chuma

NA WINFRIDA MTOI KLABU ya Simba imekamilisha safu yao ya ulinzi baada ya kumsajili beki wa kati wa Gor...

Wakili kiboko anunua kesi ya Morrison

NA WINFRIDA MTOI WAKALI aliyejizolea umaarufu nchini kutokana na uwezo na rekodi yake ya kushinda kesi kubwa nchini, Alex...

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza kupokea maombi kutoka kwa baadhi...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -