Monday, August 10, 2020

HATA TYSON ANGECHAPWA NA AJ

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

 

LOS ANGELES, Marekani

MKONGWE wa masumbwi, Larry Holmes, amesema makali aliyonayo Anthony Joshua ‘AJ’ ulingoni kwa sasa yangetosha kummaliza hata aliyekuwa bingwa wa uzito wa juu duniani, Mike ‘Iron’ Tyson.

Holmes amekuwa shabiki mkubwa wa AJ, ambaye ndiye anayeshikilia mikanda ya WBA na IBF.

Nguli huyo anamfahamu vizuri Tyson, kwani ndiye aliyekomesha rekodi yake ya kushinda mapambano 38 mwaka 1988, lakini amekiri wazi kuwa, AJ ni hatari zaidi.

“Kama angezichapa na mtu kama Mike Tyson, angeshinda tu,” alisema Holmes. Angekuwa ameshamchapa Mike Tyson kwa kwa ‘KO’. Hakuna ubishi katika hilo.

AJ, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 6, atapanda ulingoni kesho kuzipiga na bondia mwenye asili ya Cameroon, Carlos Takam, pambano litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Principality, mjini Cardiff.

Kumbe Kobe shabiki wa Spurs!

LONDON, England

ILIFAHAMIKA mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa, mkali wa mpira wa kikapu kutoka Ligi Kuu ya mchezo huo nchini Marekani (NBA), Kobe Bryant, ni shabiki wa Tottenham.

Nyota huyo alikuwa mmoja wa mashabiki waliofika kwenye Uwanja wa Wembley kutazama timu hiyo ikicheza na Liverpool.

Baada ya mtanange huo ambao Tottenham walishinda mabao 4-1, uongozi wa timu hiyo ulimkabidhi Bryant jezi yenye namba 24.

Awali, kulikuwa na tetesi kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 39, amekuwa akiishabikia Spurs tangu alipokuwa mdogo.

Kobe ni mstaafu wa kikapu baada ya kutamba NBA akiwa na Los Angeles Lakers kwa kipindi chote cha miaka 20.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -