Monday, November 23, 2020

HAWA HAPA KINA POGBA WENGINE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England

ACHANA na hat-trick ya Zlatan Ibrahimovic mchezo wa Uropa baina ya Manchester United na Saint Etienne pale Old Trafford, ulisisimua zaidi pale ndugu wawili Paul Pogba na Florentin Pogba walipokutana.

Paul kiungo mchezeshaji wa Man United, alicheza dhidi ya Florentin beki wa St. Etienne, huku mama yao mzazi akiwa ameketi jukwaani akifuatilia kwa makini pambano hilo.

Lakini unafahamu kuwa familia ya Pogba ina ndugu watatu wanaocheza soka? Mwingine ni Mathias Pogba, unajua aliko nyota huyu?

Nyota huyu kwa sasa anacheza soka nchini Uholanzi na ni raia wa Guinea, tofauti na mdogo wake Pogba anayeichezea timu ya taifa ya Ufaransa.

Makala haya yamekuandalia orodha ya ndugu 7 wa wacheza soka ambao wengine bado wako uwanjani na baadhi wameshastaafu soka kabisa.

Mathias Pogba, kaka wa Paul

Wakati pacha wake Florentin akipambana na mdogo wake Paul kwenye usiku wa Uropa pale Old Trafford, Mathias yuko kwenye jiji la Rotterdam, Uholanzi.

Mathias alizaliwa Guinea miaka 26 iliyopita, amecheza soka lake muda mwingi nchini Uingereza kwenye klabu za Wrexham, Crewe, Crawley na Partick Thistle, kabla ya kuhamia Uholanzi mwaka jana.

Paolo Suarez, kaka wa Luis

Kama ulikuwa hujui, Luis Suarez amejifunza soka kutoka kwa kaka yake Paolo aliyemzidi miaka 6.

Paolo pia amepata nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Uruguay U-20, lakini hakupata bahati ya kuichezea timu ya wakubwa.

Hivi sasa ana miaka 39, anapatikana maeneo ya El Salvador, akimshuhudia mdogo wake akiendelea kuzitikisa nyavu za wapinzani pale Nou Camp.

Giliano Wijnaldum, mdogo wa Georginio

Bila shaka umeshamwona kaka yake Georginio akiwa na Liverpool, ni kiungo wa Majogoo ya Anfield msimu huu, lakini mdogo wake Giliano Wijnaldum yeye ni winga anayekipiga kwenye klabu ya Philadelphia Union.

Ni machachari na amecheza soka lake muda mwingi nchini Uholanzi, kabla ya mwaka huu kujiunga na wakali hao wa Marekani.

Felix Kroos, mdogo wa Toni

Toni Kroos ni nyota wa Real Madrid, ana medali ya Kombe la Dunia na ni miongoni mwa viungo bora duniani, lakini mdogo wake Felix ni nahodha wa klabu ya Union Berlin inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Ujerumani.

Mafanikio makubwa ya Felix ni pale alipocheza Ligi ya Mabingwa akiwa na Werder Bremen, lakini kinyume na hapo, nyota huyo mwenye miaka 25 ameendelea kucheza ligi za madaraja ya chini.

Rodney Sneijder, mdogo wa Wesley

Hakika mzee Sneijder anayapenda mno majina ya Kiingereza na ndio sababu ya kuwapa watoto wake watatu majina ya Wesley, Jeffrey anayecheza kwenye akademi ya Ajax pamoja na Rodney.

Rodney licha ya kuwa na kipaji kikubwa cha soka, amekuwa na matatizo ya kiafya yanayomrudisha nyuma kisoka.

Tobias Schweinsteiger, kaka wa Bastian

Kwa msimu huu inaonekana kaka mtu, Tobias ana dakika za kucheza kuliko mdogo wake Bastian pale Old Trafford.

Tobias amecheza soka lake kwenye madaraja ya chini nchini Ujerumani kabla ya kuamua kutundika daluga mwaka 2015, hivi sasa ni kocha msaidizi wa timu ya vijana U-17 ya Bayern Munich.

Jonas Hummels, mdogo wa Mats

Ndugu hawa waliondoka kwa pamoja Bayern Munich udogoni, lakini ni Mats pekee aliyerejea na kucheza soka lenye kiwango cha juu.

Mdogo wake Jonas alicheza timu ya daraja la pili ya Unterhaching msimu uliopita, lakini majeraha yamemfanya aachane kabisa na soka la kulipwa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -